The House of Favourite Newspapers

JPM Apiga Magoti, Aongea kwa Uchungu Makada CCM Waliouawa – Video

0

MGOMBEA urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Chama Cha mapinduzi (CCM), Dkt. John  Magufuli, ameendelea na kampeni zake ambapo leo Septemba 29, 2020, amewasili mkoani Njombe kuomba kura kwa wananchi wa mkoa huo pamoja na kuwapigia debe wagombea ubunge wa chama chake.

 

Akiwa Makambako Njombe, Magufuli amelazimika kuwapigia magoti wananchi wa  eneo hilo wakati akiomba kura katika mkutano wake wa kampeni ikiwa ni ishara ya kuonyesha unyenyekevu kwa wananchi hao na kutambua thamani ya kura yao ambayo amewaomba wampigie kwa wingi katika uchaguzi mkuu wa Oktoba 28.

 

Leave A Reply