The House of Favourite Newspapers

JPM AZINDUA BARABARA CHUNYA, AWEKA HISTORIA – VIDEO

RAIS Dkt John Magufuli amefungua Barabara ya lami yenye urefu wa kilomita 72, inayotoka Chunya kulekea Mbya Mjini na kuahidi kuboresha zaidi miundombinu ya barabara na huduma zote muhimu katika no hilo ili wananchi wasihangaike wakati wa shughuli zao za kiuchumi na kijamii.

 

Magufuli amefanya ufunguzi huo leo Jumamosi, Aprili 27, 2019 katika Kijiji cha Mwakambona wakati akiwa njiani kulkea Chunya kwa ajili ya mkutano wa hadhara na wananchi wa wilaya hiyo ambao utafanyika leo.

 

Aidha, magufuli ameweka jie la msingi la ujenzi wa barabara ya kilomita 39 itakayotoka Chunya hadi Makongorosi na kuiunganisha Mbeya na Wilaya ya Sikonge, Tabora pamoja na Mkoa wa Singida huku akiwataka wakandarasi wa mradi huo kuongeza nguvu ili kukamilisha mradi huo mapema iezekanavyo.

 

“Zamani wakati nikiwa waziri wa ujnzi, kila nikipita mlikuwa mnaniomba barabara, sasa hivi naona hamuombi barabara tena, tutahakikisha miundombinu yote tunaiboresha, mtu atakuwa anachagua mwenyewe apite barabara ipi, hii itasaidia kuhatrakisgha shughuli zenu za maendleo ili muwe na uchumi bora, mtajirike,” amesema Magufuli.

VIDO: MSIKIE AMAGUFULI AKIZUNGUMZA

Comments are closed.