The House of Favourite Newspapers

Kagere Aamka Baada ya dk 540

0

JANUARI 26, mwaka huu kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar wakati Simba ikiifunga Namungo mabao 3-2, Meddie Kagere alifunga bao lake la 12 msimu huu kwa guu lake la kulia akimalizia pasi ya Sharaf Shiboub.

 

Baada ya hapo, Kagere alicheza mechi tano ambazo ni sawa na dakika 450 bila ya kufunga bao ikiwa ni mbele ya Coastal Union, Polisi Tanzania, JKT Tanzania, Mtibwa Sugar na Lipuli.

 

Juzi alifunga bao lake la 13 mbele ya Kagera Sugar ikiwa ni mechi yake ya sita ambayo ni sawa na dakika 540. Kagere alifunga kwa penalti kwenye ushindi wa bao 1-0 uliofanya timu yake kufi kisha pointi 59 ikikaa kileleni mwa msimamo wa Ligi Kuu Bara.

 

Leave A Reply