The House of Favourite Newspapers

Kampeni ya ‘Vuna zaidi na NBC Shambani’ Yatua kwa Walima Korosho

0
Mratibu wa uwekezaji Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Lindi Bw Gaudence Nyamwihura (aliepanda pikipiki) akijaribu ubora wa moja ya pikipiki zitakazotolewa kwa washindi wa kampeni ya ‘Vuna zaidi na NBC Shambani’ mahususi kwa wakulima wa korosho mikoa ya Lindi na Mtwara wakati wa hafla ya uzinduzi wa kampeni hiyo Mkoani Lindi mapema wiki hii. Wanaoshuhudia ni pamoja na Mkuu wa Bidhaa na Mauzo wa benki ya NBC Bw Abel Kaseko (Kulia), Meneja wa Benki hiyo Kanda ya Kusini Bi Zubeider Haroun (Katikati), Meneja wa Benki hiyo Mkoa wa Lindi Iovin Mapunda na Kaimu Mrajisi wa vyama vya ushirika Mkoa wa Lindi Bw Projestus Paschal. 

Changamoto ya huduma za kifedha iliyokuwa ikiwakabili wakulima wa korosho mikoa ya Mtwara na Lindi ikiwemo kutopata mikopo kwa wakati na makato ya fedha zao wanapofanya miamala ya kibenki, imetajiwa kuwa miongoni mwa sababu kubwa zilizopelekea wakulima hao kuvutiwa zaidi na Kampeni ya ‘Vuna zaidi na NBC Shambani’ inayoendeshwa na benki ya NBC mahususi kwa mikoa hiyo.

PIC 2 Mratibu wa uwekezaji Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Lindi Bw Gaudence Nyamwihura (katikati) akijaribu ubora wa moja ya matrekta yatakayotolewa kwa washindi wa kampeni ya ‘Vuna zaidi na NBC Shambani’ mahususi kwa wakulima wa korosho mikoa ya Lindi na Mtwara wakati wa hafla ya uzinduzi wa kampeni hiyo Mkoani Lindi mapema wiki hii. Wanaoshuhudia ni pamoja na Mkuu wa Bidhaa na Mauzo wa benki ya NBC Bw Abel Kaseko (Kulia) na Meneja wa Benki hiyo Mkoa wa Lindi Bw Iovin Mapunda. 

 

Wakizungumza wakati wa hafla ya uzinduzi wa kampeni hiyo mkoani Lindi leo, na kuhudhuriwa na wadau mbalimbali wa zao hilo wakiwemo viongozi wa kiserikali, viongozi vyama vya msingi (AMCOS) na vyama vikuu vya ushirika, wakulima hao walisema ujio wa kampeni hiyo umewahamasisha zaidi kujiunga na huduma ya NBC Shambani ili waweze kujikwamua kutoka kwenye changamoto hizo zilizotajwa kukwamisha jitihada zao za kujikwamua na umaskini kupitia kilimo cha zao hilo.

Mratibu wa uwekezaji Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Lindi Bw Gaudence Nyamwihura (wanne kushoto) akikabidhi msaada wa pikipiki iliyotolewa na benki ya NBC kwa Mwenyekiti wa Chama cha msingi (AMCOS) ya Nachunyu ya mkoani Lindi ikiwa ni msaada wa benki hiyo kwa ajili ya kurahisisha shughuli za kiutendaji kwa AMCOS hiyo. Wanaoshuhudia ni pamoja na Mkuu wa kitengo cha wateja wadogo wadogo na wakulima kutoka Benki ya NBC, Bw Raymond Urassa (wa tatu) kushoto na maofisa wengine wa benki hiyo.

 

“Pamoja na uwepo wa zawadi mbalimbali kwenye kampeni hii ikiwemo baiskeli, pikipiki, pampu za kupulizia dawa, maguta pamoja na matrekta zaidi pia tumevutiwa sana akaunti husika kwa kuwa inajibu changamoto kadhaa zinazotukabili kwenye huduma za kifedha ikiwemo ucheleweshwaji wa mikopo na makato yaliyokithiri,’’ alisema Bw Swalehe Juma, Mwenyekiti wa Nachunyu AMCOS iliyopo mkoani Lindi.

Mratibu wa uwekezaji Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Lindi Bw Gaudence Nyamwihura akizungumza na wadau mbalimbali wa zao la korosho kutoka mkoani humo wakiwemo viongozi wa kiserikali, viongozi vyama vya msingi (AMCOS) na vyama vikuu vya ushirika, wakulima wakati wa uzinduzi wa kampeni ya ‘Vuna zaidi na NBC Shambani’ mahususi kwa wakulima wa korosho mikoa ya Lindi na Mtwara.

 

Walisema changamoto ya ucheleweshwaji wa mikopo imekua ikisababisha wengi wao kupata fedha wakati usio sahihi kulingana na mahitaji yao ya kilimo na hivyo kujikuta wakitumia mikopo hiyo kwa shughuli zisizoendana na kilimo.

“Tunashukuru kuona kwamba NBC wameamua kubuni huduma mahususi kwa ajili yetu… tukiwa kama viongozi wa vyama vya msingi tumeipokea vema huduma hii na tumejipanga kuhakikisha kwamba inawafikia wanachama wetu wote kwenye maeneo yetu,’’ aliongeza.

Mkuu wa kitengo cha wateja wadogo wadogo na wakulima kutoka Benki ya NBC, Bw Raymond Urassa akitoa mafunzo kwa wadau mbalimbali wa zao la korosho kutoka mkoani Lindi wakiwemo viongozi wa kiserikali, viongozi vyama vya msingi (AMCOS) na vyama vikuu vya ushirika, wakulima wakati wa uzinduzi wa kampeni ya ‘Vuna zaidi na NBC Shambani’ mahususi kwa wakulima wa korosho mikoa ya Lindi na Mtwara.

Akizungumza zaidi kuhusu kampeni hiyo, Mkuu wa kitengo cha wateja wadogo wadogo na wakulima kutoka Benki ya NBC, Bw Raymond Urassa alisema licha ya uwepo wa huduma ya NBC Shambani kwa zaidi ya mwaka sasa benki hiyo imebuni kampeni hiyo ili kuhakikisha kila mkulima wa korosho anafikiwa na huduma hiyo ili kwa pamoja waweze kufikia adhma ya kuleta mapinduzi ya kilimo kupitia zao hilo.

PIC 6 Meneja wa Benki ya NBC Mkoa wa Lindi Bw Iovin Mapunda Mkuu akizungumza na wadau mbalimbali wa zao la korosho kutoka mkoani Lindi wakiwemo viongozi wa kiserikali, viongozi vyama vya msingi (AMCOS) na vyama vikuu vya ushirika, wakulima wakati wa uzinduzi wa kampeni ya ‘Vuna zaidi na NBC Shambani’ mahususi kwa wakulima wa korosho mikoa ya Lindi na Mtwara.

“Vuna zaidi na NBC Shambani’ ni kampeni inayolenga kuhamasisha mapinduzi ya kilimo cha korosho katika mikoa ya Lindi na Mtwara na ndio sababu hata zawadi zinazotolewa kupitia kampeni hii ikiwemo pikipiki, pampu za kupulizia dawa na matrekta zinalenga kumsaidia mkulima aweze kustawisha kilimo chake,’’ alifafanua.

Mmoja wa wadau wa zao la korosho kutoka mkoani Lindi akizungumza wakati wa uzinduzi wa kampeni ya ‘Vuna zaidi na NBC Shambani’ mahususi kwa wakulima wa korosho mikoa ya Lindi na Mtwara.

 

Akizungumza wakati akifungua kampeni hiyo kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Lindi, Mratibu wa uwekezaji Ofisi ya Mkuu wa Mkoa huo Bw Gaudence Nyamwihura pamoja na kuwasisitiza wakulima hao na AMCOS kuchangamkia kampeni hiyo, pia aliwasisitiza kubainisha vipaumbele vyao pindi wanapoamua kukopa kwenye taasisi za kifedha ili matumizi ya mikopo hiyo iwe na tija zaidi kwao.

 

Uzinduzi wa kampeni hiyo ulienda sambamba na uzinduzi wa huduma ya Bima ya afya kwa wakulima wa zao hilo inayotolewa na benki hiyo kwa kushirikiana na Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) pamoja utoaji wa msaada wa pikipiki na baiskeli zilizotolewa na benki hiyo kwa AMCOS mbalimbali za mkoa huo kwa ajili ya kurahisisha shughuli za kiutendaji kwa AMCOS hizo.

NA MWANDISHI WETU

Leave A Reply