The House of Favourite Newspapers

Kendickson uso kwa uso na Harmonize!

0

STAA wa muziki nchini Nigeria, Amu Kingsley ‘Kendickson’ amesema ana shauku ya kufanya kolabo moja na msanii wa Bongo Fleva, Harmonize kwa kile alichokiita, ana uwezo mzuri kimuziki.

Katika mahojiano maalum na mwandishi wa AMANI kwa njia ya mtandao mmoja wa kijamii, Kendickson anasema anahusudu uwezo wa galacha huyo kwenye Bongo Fleva kutoka Lebo ya Konde Gan.

Kendickson anafunguka hayo ikiwa ni siku moja tu tangu aachie ngoma yake mpya “Wayo” ambayo inatamba kwenye vituo mbalimbali vya redio ulimwenguni na mitandaoni.

“Wayo ni wimbo wangu mpya ambao nimeuachia katika mfumo wa audio na video. Watu wanaweza kuutazama mtandaoni na hasa mtandao maarufu wa YouTube. Nawashukuru sana kwa kunipokea vizuri watu wa Afrika Mashariki,” anasema Kendickson.

Akimzungumzia Harmonize, Kendickson anasema: “Ni msanii mzuri. Napenda anavyoimba. Naamini nikifanya naye kolabo moja, nitazidi kubamba katika ukanda huu wa Afika Mashariki. Nataka kupanda mizizi yangu hapa Afrika Mashariki.”

Wayo uliotayarishwa na prodyuza mkali wa Kinigeria, Insane Chips upo kwenye mahadhi ya Afrobeat ambapo Kendrickson anaimba kwa hisia akizionyesha kwa mpenzi wake.

Akiendelea kuzungumzia wimbo huo, Kendickson anasema: “Nataka kuwahakikishia mashabiki wangu wote na hasa wa Afrika Mashariki kuwa, nimekuja kuwapa muziki mzuri. Naamini wimbo huu mtaupenda wana- Afrika Mashariki.”

Kendrickson ni mkali wa mahadhi mbalimbali kama Afrobeat, Hip Hop na mingine.

Stori: Mwandishi Wetu

Leave A Reply