The House of Favourite Newspapers

Kiba akataa saluti ya Diamond!

0

ali kibaMusa Mateja, Risasi Rumamosi

Dar es Salaam: Zile habari njema kuwa bifu lililofukuta kwa muda mrefu kati ya mastaa wawili wa Afro-Pop, Ali Saleh Kiba ‘King Kiba’ na Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ limekwisha, zimechukua sura mpya ikiwa ni wiki mbili tangu Diamond alipoamua ‘kusarenda’ kwa Kiba na kumpigia saluti.

Mara baada ya habari ya Diamond kumpigia saluti Kiba kuruka kwenye ukurasa wa mbele wa gazeti hili wiki mbili zilizopita, ndipo zikaibuka ‘rumazi’ kwamba Kiba alichomolea nje saluti hiyo.

diamondALICHOKISEMA DIAMOND

Katika mazungumzo yake na gazeti hili, Diamond alifunguka: “Kiba namkubali, namheshimu. Ni miongoni mwa mastaa walionitangulia, saluti kwake. Lakini si yeye tu, kuna wasanii wengi ninaowaheshimu kwa kazi zao, wapo wengi tu wenye mchango mkubwa, saluti kwao.”

Kwa mujibu wa chanzo hicho, Kiba alikataa saluti hiyo kwa madai kwamba kiti cha ufalme wa Bongo Fleva ni chake na hakijawahi kuchukuliwa na mtu yeyote na kwamba labda kilipata vumbi tu lakini akarejea kisha akakifuta na kukikalia.

ALICHOKISHANGAA KIBA

“Alichoshangaa Kiba ni kwamba, yeye ndiye mfalme wa Bongo Fleva na kiti chake hakijawahi kukaliwa na mtu sasa Diamond alikuwa wapi kulijua hilo na mbaya zaidi msisitizo wake ni uleule kwamba yeye ni levo tofauti, sasa iweje alinganishwe na mtu ambaye siyo wa levo zake?

“Kiukweli ile kauli ilimtibua sana Kiba maana alishakataa kulinganisha vitu ambavyo havifanani,” kilisema chanzo hicho.

Hata hivyo, chanzo kingine kilidai kuwa siyo kwamba Kiba hataki kufanya kolabo na Diamond kwa sababu kabla ya mambo hayo waliwahi kushirikiana lakini Diamond akafuta vesi za Kiba.

“Ndiyo maana Kiba alipokutana na Sallam (mmoja wa mameneja wa Diamond) walizungumza vizuri kabisa kuonesha kwamba hilo halina tatizo.

WANACHOKATAA TEAM KIBA

“Wanachokataa Team Kiba (kundi la mashabiki wa kufa wa Kiba kwenye mitandao ya kijamii) ni kitendo cha Diamond kujiona yupo levo moja na Kiba au wakati mwingine timu yake (Team Diamond) kudai kuwa yupo juu kimataifa kuliko mtu wao (Kiba),” kilinyetisha chanzo hicho.

TEAM DIAMOND WATANGAZA VITA MPYA

Kwa upande wao, Team Diamond kwenye mitandao ya kijamii walishangazwa na mjadala ulioibuliwa na Team Kiba kwamba ‘bosi’ wao huyo amekataa saluti ya Diamond na kwamba huwa hapendi kumzungumzia kwa kuwa si levo yake.

“Huyu Kiba anachokoza nyuki walioko kwenye mzinga, Chibu (Diamond) amejishusha sana kwake na kumkubali lakini yeye analeta mapozi. Sasa atatujua sisi ni akina nani na kama anadhani anaweza kumfunika Chibu basi ajue imekula kwake. Ndiyo kwanza tunazidi ‘kushaini’ kimataifa,” ilisomeka sehemu ya maoni mengi ya Team Diamond kwenye mitandao ya kijamii.

KIBA ATOA LA MOYONI

Baada ya kunyetishiwa sakata hilo lililoaminika kuwa limekwisha, gazeti hili lilizungumza na Kiba ambaye hata hivyo alithibitisha madai ya chanzo chetu kuwa hapendi kumzungumzia Diamond akigoma kutaja jina lake na kumuita mtu huyo.

“Kama kuna jambo lingine niulize lakini sipendi kumzungumzia mtu huyo,” alisema Kiba kwa kifupi na hata alipobanwa zaidi hakuwa tayari kumzungumzia Diamond.

TUMRUDIE DIAMOND

Kufuatia majibu hayo, gazeti hili lilimrudia Diamond na kumweleza kinachoendelea juu yake na Kiba ambapo naye alijibu kwa kifupi kuwa alionesha kumkubali Kiba kiroho safi lakini kama amemchomolea, basi yeye anamwachia Mungu.

“Sina kinyongo na mtu, kama ameamua hivyo mimi namwachia Mwenyezi Mungu,” alisema Diamond.

TULIKOTOKA

Diamond na Kiba wamekuwa katika bifu ‘kroniki’ la msimu ambapo kuna wakati huwa linapoa na wakati mwingine huwa linashika kasi kama ilivyo kwa sasa.

Leave A Reply