The House of Favourite Newspapers

Kiba: Sikumwalika Shilole

0

SIKU chache baada ya mwanadada Esha Buheti kutangaza kujiweka kando kumsapoti Alikiba kwa kile alichodai kutothaminiwa na mwanamuziki huyo licha ya kumpa ushirikiano katika kazi zake mbalimbali, kufuatia sintofahamu ya hivi karibuni kwenye uzinduzi wa albamu mpya ya msanii huyo ambapo kwa mujibu wa Esha ni kuwa aliwapa nafasi na thamani watu ambao hawana mchango kwenye kazi zake akiwemo Shilole ambaye alipewa kipaumbele kwenye tukio hilo.

 

Alikiba amemjibu tuhuma hizo na kusema; “Kuna vitu ambayo vinaharibu sana watu haya mambo ya Social Media, watu wanataka credit sana.

 

“Dada yangu Esha Buheti kwa sababu amekuwa kwenye vitu vyangu vingi na nimekuwa nikizungumza naye vitu vingi iwe cha kishenzi au kistaarabu lakini amenistaajabisha sana kwa sababu hajaona thamani niliyompa ya kumuweka karibu na familia yangu, nasikitika sana, Esha sio shabiki wangu ni familia yangu.

 

“Ana connection na familia yangu mama na mke wangu, huwa anakuja nyumbani mara kwa mara. Furaha yangu ya kufanya jambo langu pale Serena watu wengi wameitikia. Na ile furaha yangu na jambo limekwenda vizuri siwezi kukumbuka kila mtu nilimsahau hadi Aidan Charlie meneja wangu,” alisema Alikiba.

 

Msanii huyo pia ameikanusha kuwa alimpendelea Shilole anayedaiwa kupewa nafasi ambayo ilitakiwa apewe Esha Buheti.

 

“Kama kuna mtu ana bifu naye alialikwa mimi sikumwalika huyo mtu. Sikumwalika Shilole nilishtukia tu yupo pale ukumbini na nisingeweza kumkumbuka Shilole kwa sababu sina mazoea naye. Esha namkumbuka sana. Hata unilazimishe vipi nisingeweza kumkumbuka Shilole hatupo karibu kabisa,” aliongeza Alikiba.

Leave A Reply