The House of Favourite Newspapers

Kibajaji Amtaka Ndugai Ajiuzulu

0

Mbunge wa Mtera na Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chama Cha Mapinduzi CCM (NEC), Mhe. Livingstone Lusinde ‘Kibajaji’ amemtaka Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Job Ndugai ajiuzulu wadhifa wake huo ili awaachie watu wengine.

 

Lusinde ameyasema hayo leo, Januari 6, 2022 kufuatia kitendo cha Ndugai cha kupinga mkopo wa shilingi Trilioni 1.3 uliokopwa na Rais Samia Suluhu Hassan.

 

“Nikiwa kama Mbunge wa Mkoa wa Dodoma, nikiwa kama Mkazi wa Mkoa huu, nikiwa kama Mgogo nasema Spika Ndugai amefanya kosa kubwa sana, namshauri leo asisubiri Kesho ajiuzulu isifike kesho awe amejiuzulu nafasi ya Uspika wa Bunge.

 

“Kuomba msamaha duniani unapaswa kusema maneno machache” nisamehe nimekosea”ukipitia hotuba ya Ndugai anakanusha akisema clip imeungwa, hakusema. Hata anayemuomba radhi hawezi kuchukulia serious kwamba unaomba radhi. Ni kama kumkanyaga mtu akatoa damu ukawa unacheka.

 

“Ukiitazama clip ya Ndugai hamna hata kipande kilichokatwa anawasukumia waandishi eti wamekata sio kweli, Ndugai ni kaka yangu anajua nampenda kazi nilianzia Jimboni kwake lakini kujiuzulu kwake kutatupa faida kubwa sana ya kuendelea kuheshimika.

 

“Mhe Rais Samia usije kudhani sisi tupo pamoja na Ndugai katika kukusema, kukusimanga na kukunyanyasa katika maendeleo makubwa unafanya. Watanzania mnisamehe kwa kuchelewa kusema Nilikuwa najiridhisha kwa nini Rais mwenye huruma kama Hangaya anachelewa kumsamehe Job,” amesema Lusinde.

Leave A Reply