The House of Favourite Newspapers

Kifo Cha Kanumba Kilivyomtoa Ray Mchezoni

0

MWANZONI mwa miaka ya 2000, huu ushindani unaoshuhudiwa kwenye muziki kati ya Diamond Platnumz na King Kiba au Harmonize ulikuwa kwenye Bongo Movies kati ya Kanumba na Ray.

Miaka hiyo, Kanumba na Ray waliteka sebuleni za wapenzi wa filamu za Kibongo huku kukiwa na mabishano makubwa ya nani ni zaidi ya mwingine.

Kila mmoja alikuwa na kijiji chake ambacho kiliendesha propaganda kuonesha kila mmoja ni zaidi ya mwingine.

Hata hivyo, kifo cha Kanumba siku ile ya Aprili 7, 2012 kilikuwa ni pigo kubwa kwa Ray na bado kimebaki kuwa pigo kwani kinatajwa kumtoa kabisa Ray kwenye mchezo na hana maajabu tena.

Kwa kifupi Kanumba ndiye alikuwa ameshikilia nyota ya Ray; jamaa alikuwa anapenda mno kuigiza.

Leave A Reply