The House of Favourite Newspapers

Kikwete Aongoza Mamia Kumuaga Anna Senkoro

1

Rais Mstaafu, akiweka udongo kwenye kaburi la marehemu Senkoro.

2

Rais Mstaafu, Kikwete aliongozana na mkewe, Mama Salma Kikwete. Pichani akiweka udongo kwenye kaburi la marehemu Senkoro.

3

Watoto wa marehemu, wakiongozwa na Joan Jafet (aliyesimama) wakiweka udongo kwenye kaburi la mama yao.

4

Waombolezaji wakiwa kwenye misa ya mwisho ya kumuombea marehemu, iliyoongozwa na Pastor Samuel Adeyemi (wa kwanza kushoto).

5

Jeneza lenye mwili wa marehemu likiwa tayari limeshaingizwa kwenye nyumba yake ya milele.

6 7 8 9 10

Katibu wa Itikadi na Uenezi wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Humphrey Polepole akiwa na spika mstaafu, Anne Makinda, katika Kanisa la Winners Chapel International, Banana Ukonga kwenye ibada ya kumuaga marehemu.

 

 

11 12 13 14 15 16 17 18

Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne, Jakaya Mrisho Kikwete, leo amewaongoza mamia ya waombolezaji katika mazishi ya aliyekuwa mgombea urais wa kwanza mwanamke, Anna Senkoro aliyefariki Januari 4, 2017 katika Hospitali ya Muhimbili, baada ya kusumbuliwa na maradhi ya moyo kwa muda mrefu.

Mazishi yamefanyika katika Makaburi ya Kinondoni ambapo awali, ilifanyika ibadaya kumuombeamarehemu, iliyofanyika katika kanisa la Winners Chapel International, Banana Ukonga na kuhudhuriwa na wanasiasa mbalimbali, wakiwemo Humphrey Polepole ambaye ni Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Anne Makinda, spika mstaafu huku Ukawa wakiwakilishwa na Makongoro Mahanga.

Katika Uchaguzi Mkuu wa 2005, marehemu Senkoro alijitokeza kuwania urais, akipambana na Kikwete kwa tiketi ya Chama cha PPT- Maendeleo, na kuweka historia ya kuwa mwanamke wa kwanza Tanzania kuwania nafasi hiyo, tangu kuanzishwa kwa mfumo wa vyama vingi.

Marehemu ameacha watoto watatu na wajukuu wawili. Mungu ailaze mahali pema peponi roho ya merehemu. Amina.

 

Comments are closed.