The House of Favourite Newspapers

Kisa sms… Lindsay, baby wake wazinguana kinoma shereheni

0
Picture Shows: Egor Tarabasov, Lindsay Lohan June 22, 2016 Celebrities arrive at the Caudwell Childrens Charity Butterfly Ball at Grosvenor House Hotel in London, England. Non Exclusive WORLDWIDE RIGHTS Pictures by : FameFlynet UK ¿ 2016 Tel : +44 (0)20 3551 5049 Email : info@fameflynet.uk.com
Picture Shows: Egor Tarabasov, Lindsay Lohan June 22, 2016 Celebrities arrive at the Caudwell Childrens Charity Butterfly Ball at Grosvenor House Hotel in London, England. Non Exclusive WORLDWIDE RIGHTS Pictures by : FameFlynet UK ¿ 2016 Tel : +44 (0)20 3551 5049 Email : [email protected]

Muigizaji Lindsay Lohan juzikati alijikuta akidata baada ya kuona ujumbe wa kimapenzi kutoka kwa mwanamke mwingine kwenye simu ya mpenzi wake aitwaye Egor Tarabasov, hali iliyoibua ugomvi.

Wawili hao walikuwa wamekwenda kwenye Kisiwa cha Mykonos kulikokuwa na sherehe lakini ghafla furaha yao ikaingiwa na mdudu.

Egor Tarabasov AND lANDRY (2)Inaelezwa kuwa, wakati wapenzi hao wakiendelea kula bata huku mama wa Egor akiwa karibu yao, Lindsay aliona sms ambayo haikumfurahisha, kwa hasira aliichukua simu ya mpenzi wake na kuitupa baharini.

Kitendo hicho kilimfanya Egor kumkunja na kummwagia Lindsay kinywaji, hali iliyomfanya mama wa Egor kusikitika na kuondoka huku Lindsay naye akienda kupanda gari na kuondoka zake.

Baadaye Lindsay aliandika kwenye ukurasa wake wa Instagram kuwa mapenzi yanaua hasa ukiwa mtu mzima na ukapitia mazito.

 

Leave A Reply