The House of Favourite Newspapers

KISUTU: Kesi ya Aveva na Kaburu Yasogezwa Mbele

0
Godfrey Nyange ‘Kaburu’ akifikishwa mahakakani leo.

Kesi ya madai ya utakatishaji fedha inayowakabili viongozi wa Simba, Rais Evans Aveva na Makamu wake, Godfrey Nyange ‘Kaburu’ imeahirishwa kusikilizwa leo Julai 31 katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam hadi kutokana na upelelezi kutokamilika.

 

Aveva akishuka kwenye gari la magereza

 

Kesi hiyo iliyokuwa isikilizwe na Hakimu Victoria Nongwa imepamgwa kusikilizwa tena Agosti 7 mahakamani hapo, ambapo watuhumiwa wamerudishwa gerezani.

Aveva na Kaburu wanakabiliwa na tuhuma za kughushi nyaraka za Klabu ya Simba na kutakatisha dola 300,000 (zaidi ya Sh milioni 650) na wamekuwa rumande tangu Juni 29, mwaka huu.

 

NA DENIS MTIMA | GLOBAL PUBLISHERS

 

Kimenuka Simba wazee hawataki Mabadiliko, wakataa mkutano

Leave A Reply