The House of Favourite Newspapers

Kitoto Kichanga Chatupwa Kichakani

0

MTOTO wa siku moja mwenye jinsia ya kike, amekutwa ametupwa kwenye kichaka [akiwa amefariki ]katika kata ya mlimba, tarafa ya mlimba halmashauri ya mlimba mkoani morogoro na kutofahamika mara moja mtu aliyefanya kitendo hicho.

 

Akizungumza mwandishi, Ofisa Mtendaji wa Kata ya Mlimba, Mhenga Acley , amesema kuwa tukio hilo limetokea Februali 16, 2020 majira ya saa tatu asubuhi, katika kitongoji cha barabara mpya kata Mlimba

Bwana mhenga alisema kuwa kuna mpita njia alikuwa anapita barabarani ambaye aliouona mfuko wa salufeti ambao alitaka kuokota mfuko huo, ambapo baada ya kuangalia mfuko huo ghafla aliona kiumbe hicho kilichowekwa ndani ya mfuko huo.

 

Naye mwenyekiti wa kitongoji cha barabara mpya kata ya Mlimba amesema kuwa amesikitishwa na tukio hilo kutokea kwa tukio hilo katika kitongoji chake.

 

Hata hivyo wakizungumzia tukio hilo wakazi wa kitongoji hicho wameelezea hisia zao juu ya kutupwa kwa kiumbe hicho katika eneo hilo nakuomba serikali kumtafuta mhusika aliyefanya kitendo hicho. Jeshi la Polisi limethibitisha kutokea kwa tukio hilo na upelelezi unaendelea.

Leave A Reply