The House of Favourite Newspapers

Kituo cha Biashara na Hoteli Angani Kuzinduliwa

0

UNAAMBIWA Kampuni maarufu duniani ya Utalii wa angani ya Blue Origin ambayo inamilikiwa na bilionea wa dunia ambaye ni mmiliki wa Kampuni ya Amazon, Jeff Bezos, imetangaza mpango wake wa kuzindua kituo cha biashara cha angani kitwacho Orbital Reef.

Kukamilika kwa kituo hicho kutawapa wateja nafasi ya kutengeneza filamu katika eneo hilo, kufanya shughuli mbalimbali za utafiti ambapo pia kitakuwa na hoteli ya angani.

Bezos amesema wanatarajia kianze kufanya kazi kufikia mwisho wa muongo huu na watashirikiana na kituo cha angani cha Sierra na Boeing ili kujenga kituo hicho chenye ukubwa wa futi 32,000.

 

Katika mkutano na wanahabari kuzindua mpango huo, maafisa wakuu wa Blue Originna kituo cha angani cha Sierra walikataa kutoa gharama ya ujenzi wa kituo hicho, ijapokuwa inadaiwa wanahakika kupata ufadhili wa kitita kikubwa kutoka kwa bwana Bezos, ambaye amejitolea kutumia $1bn (Tsh trilioni 2.3) kwa mwaka katika kampuni ya Blue Origin.

 

Tangazo hilo linajiri huku Nasa ikitafuta mapendekezo ya kuunda kituo mbadala ili kuchukua mahala pake majengo ya kituo hicho yalio angani kwa miaka 20.

Leave A Reply