The House of Favourite Newspapers

Kocha: Kiduku Anahitaji Bondia wa Nje

0

KOCHA wa bondia wa ngumi za kulipwa nchini, Twaha kiduku, Chanzi Mbwana amefunguka kuwa kwa sasa bondia wake yupo tayari kwa pambano lolote haswa kupambana na bondia atakayetokea nje ya nchi.

 

Akizungumza na Championi Jumamosi, Mbwana alisema: “Lengo letu ni kukuza nyota za bondia wetu, ambaye kwa sasa ana nyota mbili na nusu. Tunahitaji wapambanaji na mabondia kutoka nje zaidi ambao wana nyota kubwa kwani kwa kufanya hivyo uwezo na umaarufu pia utaongezeka.

 

“Tupo tayari kuanzia sasa kwa pambano lolote la nje kwani bondia wetu Twaha amekwisha pumzika vya kutosha na mazoezi mengi pia, tunasubiri tu wadhamini wajitokeze tufanye kazi.”

MOHAMED TELU NA LILIANI CHULA (TUDARCo)

Leave A Reply