The House of Favourite Newspapers

Kocha Mkuu wa Misri yamkuta, Kuikosa Fainali ya AFCON

0

Kocha mkuu wa Timu ya Taifa ya Misri, Carlos Queiroz amefungiwa michezo miwili na kutozwa faini ya dola 10,000 kufuatia kadi nyekundu aliyoonyeshwa jana katika mchezo wao wa nusu fainali dhidi Cameroon.

Kocha Queiroz atakosa mchezo wa fainal ya AFCON 2021 dhidi ya Senegal na mchezo wa mkondo wa kwanza wa mchujo wa kufuzu Kombe la Dunia dhidi ya Wasenegal hao.

Kocha huyo atarejea kusimama kwenye touchline katika mchezo wa marejeano wa kufuzu kwenda kombe la Dunia dhidi ya Senegal.

Leave A Reply