The House of Favourite Newspapers

Wolper: Tupunguze Mazoea Ya Hovyo

0

Staa wa filamu na pia mwanabiashara kutoka Tanzania, Wolper amewataka mashabiki wake na binadamu wote kwa jumla kupunguza kuzoeana na watu hovyo.

 

Kupitia ujumbe wake ambao ameuchapisha katika ukurasa wake wa Instagram, Wolper amesema kwamba kuna baadhi ya watu tunawapa nafasi katika maisha yetu na kuwachukulia kama rafiki ila baadaye wanatuchukulia poa na kutufanyia madharau.

 

“Kama kuna kitu kinazidi kuwa somo kwenye maisha ninayoishi. Ni kupunguza mazoea na watu (kuzoeana)….Mazoea huzaa mambo mengi….Imagine leo ungekuwa hujazoeana na yule aliyekuumiza, angepata wapi nafasi ya kukuumiza kama ungekuwa haujamzoea?” ameandika Wolper.

 

Amesisitiza kuwa adui wengi ni watu ambao tuliwapa nafasi katika maisha yetu ila baadaye wakfanya mazoea ya kuchukiza.

 

Wolper amewarai watu kuangazia zaidi jinsi wanaweza kuboresha maisha yao badala ya kujenga urafiki ambao baadaye unakuja kuwaletea balaa.

CC; @sifaelpaul

Leave A Reply