The House of Favourite Newspapers

Kocha Yanga: Wachezaji Simba ni wavivu

0

CHARLES Boniface Mkwasa, Kaimu Kocha Mkuu wa Yanga, amesema kuwa kilichowaponza Simba kushindwa kulinda mabao yao mawili waliyofunga juzi Uwanja wa Taifa, ni uvivu wa wachezaji wake kiujumla.

 

Simba iliwakaribisha Yanga kwenye mechi iliyosubiriwa kwa hamu kubwa na mashabiki wao ila waliambulia sare ya kufungana mabao 2-2, licha ya Simba kuanza kufunga mabao yote mawili.

 

Mkwasa alisema kuwa alitambua udhaifu wa wachezaji wa Simba ni uvivu na kutokuwa na uwezo wa kuhimili mikikimikiki kwa dakika 90, jambo lililofanya awabane mbavu kipindi cha pili.

 

“Ukiachana na aina ya timu niliyokuwa nacheza nayo kutegemea penalti pia wachezaji wake ni wavivu kwenye suala la ubora wao na utimamu jambo ambalo lilinifanya nikabadili mbinu kipindi cha pili, nilijua kwamba lazima watachoka na watashindwa kwenda na kasi ambayo nitawapeleka.

 

“Nilishindwa kwenda nao kipindi cha kwanza kwa kasi yao ili kuwasoma. Kulikuwa na uwezekano wa kuwafunga kabisa, bahati muda haukutosha,” alisema Mkwasa.

LUNYAMADZO MLYUKA, Dar es Salaam

Leave A Reply