testiingg
The House of Favourite Newspapers

Korona Yamshika Vibaya Lupita Nyong’o Aisee

0

MWIGIZAJI wa Hollywood na Mshindi wa Tuzo ya Oscar, Lupita Nyongo mwenye asili ya nchini Kenya amejikuta kwenye maumivu makali baada ya kushikwa pabaya na virusi vya Korona au UVIKO-19.

Lupita; kupitia ukurasa wake wa Twitter anasema kuwa, alipimwa na kupatikana na virusi hivyo vya Korona licha ya kupata chanjo.

Katika maelezo yake, Lupita anasema kuwa, kwa amejitenga na watu kuzuia kueneza virusi hivyo na anatarajia kupata nafuu hivi karibuni.

“Mimi pia nimethibitishwa kuwa na COVID-19. Nimechanjwa kikamilifu. Nimejitenga na ninaamini nitakuwa mzima.”

Lupita ni miongoni mwa waigizaji waliotarajiwa katika tamasha la kusisimuliwa lililotarajiwa kufanyika Ijumaa iliyopita, lakini hakuweza kuhudhuria.

Leave A Reply