The House of Favourite Newspapers

Kufuru za Mondi kwa Zuchu Zaibua Tafrani

0

NI yeye! Ndiyo, ni yeye Tanasha Donna ambaye ametengeneza habari mpya kufuatia kuona mzazi mwenzake Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ anamfanyia kufuru za kufa mtu, msanii mpya wa Wasafi Classic Baby (WCB), Zuhura Kopa ‘Zuchu’, IJUMAA WIKIENDA linakupakulia uhondo.

 

Hivi karibuni, Diamond au Mondi alimsaini Zuchu kwenye lebo yake ya Wasafi na tangu hapo amekuwa akimfanyia kufuru za hapa na pale, kiasi cha kudaiwa kumtibua Tanasha.

 

NI MUDA MFUPI TU…

Ndani ya muda mfupi, Zuchu ndiye habari ya mjini kufuatia promo kubwa anayopewa na Mondi ambaye Tanasha hakufanyiwa hata robo yake alipokuwa na jamaa huyo.

Uchunguzi wa Gazeti la IJUMAA WIKIENDA umenasa picha mbalimbali ambazo zinamuonesha Tanasha akiponda raha huku akifanyiwa kufuru za shopping kwenye maduka makubwa (malls) jijini Dar.

 

ATUMIA NDINGA LA TANASHA

Kama hiyo haitoshi, kuna picha ambazo zinasadikika kuwa Mondi alitoka yeye, mama yake mzazi na kampani ya kutosha huku Zuchu akijivinjari kwenye lile ndinga linaloaminika lilikuwa ni la Tanasha, Toyota Land Cruiser V8.

 

“Mtoto sasa hivi mambo mazuri, apewe nini tena. Anafanyiwa ma-shopping ya nguvu, anaishi mahali pazuri, lakini kama hiyo haitoshi, anatumia mpaka ndinga lile la Tanasha lenye thamani ya shilingi milioni 150,” kilieleza chanzo makini kilicho ndani ya Wasafi.

 

FULL KUPOSTIWA

Aidha, Mondi amekuwa akimposti Zuchu kila wakati kwenye kurasa zake za mitandao ya kijamii hususan Instagram yenye wafuasi milioni 9.2, jambo ambalo limemfanya binti huyo wa Malkia wa Mipasho Afrika Mashariki na Kati, Khadija Kopa kuonekana ni ‘lulu’ kwenye Lebo ya Wasafi.

 

Nyimbo zote alizotoa Zuchu kuanzia Hakuna Kulala, Nisamehe, Raha, Ashua akiwa amemshirikisha Mbosso, Wana, Kwaru na Mauzauza aliyomshirikisha mama yake, Khadija Kopa; zimepokelewa vizuri na tayari zina rundo la watazamaji (views) kwenye mitandao ya kijamii na kuweka rekodi mbalimbali ndani na nje ya Bongo.

 

TANASHA AKINUKISHA

Baada ya Tanasha kushuhudia kufuru hizo kwenye mitandao ya kijamii akiwa nchini kwao Kenya, amekinukisha kwa kuzungumza na vyombo mbalimbali vya habari nchini humo.

 

Tanasha amekaririwa akisema, anamshangaa Mondi kuyafanya anayoyafanya kwa sasa kwa Zuchu kuonesha kwamba anamsaidia mtoto wa kike wakati kiuhalisia siyo mtu wa hivyo.

 

“Inanishangaza kuona mwanaume asiyejali wanawake anajifanya anawasaidia. Kitu bandia huwa siku zote hakijifichi. Ni kama begi bandia, madini bandia yataishi kwa siku kadhaa pengine wiki au miezi, lakini baadaye kila mtu atajua ni bandia,” alikaririwa Tanasha.

 

TAFRANI KAMA YOTE

Kitendo cha Tanasha kuweka ujumbe huo, tafrani ilikuwa kubwa kwenye mitandao mbalimbali ya nchini Kenya, watu walianza kuporomosha matusi mazito.

 

Kuna ambao walimtukana Mondi kwa kumzalisha Tanasha kisha kumuacha na sasa kujifanya anamsaidia Zuchu kimuziki wakati alishindwa kumsaidia Tanasha ambaye mbali na kuwa mwanamuziki, alikuwa mzazi mwenzake.

 

WENGINE WAMTETEA MONDI

Hata hivyo, kundi lingine liliibuka na kumtetea Mondi kwa maelezo ya kuwa Tanasha hana budi kukaa kimya maana muda wake umeshapita, hivyo asitegemee msaada tena kwa Mondi.

Kundi hilo lilisema, Tanasha alishaanza kusaidiwa alipokuwa na Mondi, lakini kwa kuwa penzi lilikufa basi na biashara yake iliishia hapo.

 

Mitandao mbalimbali nchini Kenya iliripoti juu ya tafrani hiyo ambapo walieleza jinsi watu walivyokuwa na hasira kufuatia Mondi kujionesha kuwa ni mwema sana kwa Zuchu wakati huu wakati alishafanya hivyo kwa wanawake wengine kisha akawaacha solemba.

 

Gazeti la IJUMAA WIKIENDA liliwatafuta Mondi na Tanasha ili kupata undani zaidi wa stori, lakini wote wawili simu zao ziliita bila kupokelewa na hata walipotumiwa chatting za WhatsApp zilionesha kusomwa, lakini hawakujibu hivyo jitihada zinaendelea.

 

WAPENZI WA ZAMANI WATAJWA

Mitandao hiyo ilisema, Mondi alifanya hivyo kwa mastaa wa Kibongo, Wema Isaac Sepetu, Hamisa Mobeto, Penniel Mungilwa ‘Penny’ na Zarinah Hassan ‘Zari The Boss Lady’ alipokuwa nao kwenye uhusiano, lakini hata hivyo, wote aliwaacha solemba.

 

ZUCHU NI NANI?

Zuchu ni msanii wa pili wa kike kusainiwa kwenye Lebo ya Wasafi baada ya dada yake Mondi, Queen Darleen.

Tangu Zuchu asajiliwe hivi karibuni, amekuwa akipewa kipaumbele kimuziki, jambo ambalo limezua maswali na wengine kumsihi Zuchu kuwa makini asije akaingia kwenye himaya ya mapenzi ya msanii huyo kwani mwisho wake hautakuwa mzuri.

 

Baada ya kuanza kutangazwa na Mondi kama msanii wake mpya, tayari amevuna wafuasi zaidi ya laki mbili Instagram huku akaunti yake ya YouTube ikiwa na wafuasi zaidi ya laki moja.

STORI: MWANDISHI WETU, DAR

Leave A Reply