The House of Favourite Newspapers

Kumbe Tommy na Lyyn Ilikuwa Kweli

0

MKALI mwingine wa Bongo Fleva anayetumikia Lebo ya Kings Music, Tommy Flavour amefunguka kuwa, kumbe penzi lake na video vixen Lyyn lilikuwa ni la kweli na siyo kwa ajili ya kujipandisha kimuziki.

 

Tommy amekunusha madai kwamba, Lyyn alilipwa pesa ndefu ili wafanye kiki kwa ajili ya ku-push (kusukuma) muziki wao.

“Haikuwa hivyo, ingekuwa hivyo hata King (Kiba) asingeruhusu, anaheshimu sana watu ambao anafanya nao kazi, kwa hiyo hakusema kitu kwa sababu alijua ukweli wa jambo hilo.

 

“Baadaye sikuona faida ya kuyahusisha mambo hayo na mitandao, lakini siyo kwamba kuna kitu chochote kilihusika nyuma ya pazia au alilipwa pesa kama watu wanavyosema, siyo kweli,” anasema Tommy ambaye albam yake imekamilika kila kitu akisubiri muda tu ufike aachie mzigo hewani.

 

Kabla ya hapo, Lyyn ambaye aliuza sura kwenye Video ya Kwetu ya Rayvanny, aliwahi kudaiwa kutoka kimapenzi na kaka mkubwa kunako Bongo Fleva, Diamond Platnumz.

STORI; KHADIJA BAKARI, DAR

Leave A Reply