The House of Favourite Newspapers

Zuchu ‘Paka’ Kiboko ya ‘Simba’ Mondi

0

KUPISHA njia ni kukubali kuzidiwa kasi; lakini si kukubali kushindwa kwa sababu safari ina mengi njiani. Zuchu msanii aliyesainiwa na Lebo ya WCB inayomilikiwa na Diamond mwaka mmoja uliopita kasi yake ya sanaa inaonekana ni kubwa.

 

Kuna watu wameanza kusema Diamond anapaswa kumpisha njia msanii huyo wa kike asongeshe gemu lake, ingawa ni kwa faida ya Lebo.

 

Hata kama Diamond ni mkubwa kwenye Lebo yake ya WCB lakini tawimu mitandaoni za kisanii zinamfanya aonekane mdogo kwa Zuchu ni kama paka kumzaba vibao simba.

 

Mondi alianza kutisha kisanii mwaka 2013 na ngoma yake ya Mbagala, Nitarejea na Kamwambie, hesabu zinampa miaka zaidi ya Saba kwenye hit song Bongo.

 

Lakini pamoja na ujanja wake wote Diamond hakuwahi kuishika dunia ya muziki hasa kwenye mitandao ya kijamii kwa ngoma yake bila kushirikisha wasanii wengine.

 

Katika maisha yake, ngoma pekee ambazo Mondi anaweza kusema angalau zimemfanya atishe mitandaoni ambako dunia ya sasa inaishi ni mbili kama sikosei, Sikomi na Jeje nyingine ngoma nyingine za Diamond zinazotamba ni kolabo.

 

Sikiliza rekodi hii; Zuchu ambaye mwanzo alianza kubezwa kwamba anabebwa na Diamond; ndani ya mwaka mmoja ameweza kutikisha kwenye mitandao ya kijamii kwa kupaisha ngoma yake ya Sukari hadi anga za mbali.

 

Zuchu alipoachia Sukari yake Januari 2020, akisimama mwenyewe kwenye shoo, ngoma hiyo imekuwa sukari kweli kwa watu na kuweza kufikisha watazamaji Mil 55.8 hadi makala hii inaandikwa.

 

Ngoma ya Diamond Sikomi aliyoachia Desemba 6, 2017 mpaka sasa imetazamwa na watu Mil52.8, sijui unaelewa takwimu hizi au mwalimu andelee kukuelewesha.

 

Ngoma nyingine ya Mondi inayomuweka kifua mbele ni Jeje aliyoifyatua Februari 26, 2020 ambayo imetazamwa na watu Mil57. Vipi una lolote la kusema kwa Diamond au unamshauri kitakwimu apishe njia?

 

Hata hivyo sifa ya kipekee ambayo Diamond anabeba begani mwaka ni kuwa msanii mwenye Lebo ambayo imeweza kutoa wasanii wengine wakubwa nchini. Lebo nyingine ni kama zinajipikilisha chakula cha kitoto kwa lugha ya kwetu.

 

Hakika mti hauwezi kuwa mkubwa bila kuwa na matawi, pengine hii ndiyo tofauti kati ya WCB na Lebo nyingine hapa Bongo.

 

Hata hivyo, kuna baadhi ya watu wanaitazama kasi ya Zuchu kuwa nayo huenda ikamfanya achepuke njia baada ya kujiona amepishwa safarini na bosi wake Diamond.

 

Harmonize alipokuwa na kasi kubwa WCB na kupewa nafasi ya kutanguliwa alipinda kona akaenda kuanzisha Lebo yake ya Konde Gang, bahati yake hakupotea mazima.

 

Rayvanny naye anatajwa kuanzisha lebo yake lakini hii isiwe sababu ya kuwafanya wasanii wengine kama Zuchu, Mbosso nao kuvimba vichwa na  kujiona kuwa wanaweza kutembea kwa miguu yao kisa tu wamepata watu wa kuwapigia makofi na kuwaimbia nyimbo za “kasimama peke yake.”

Na Richard Manyota

Leave A Reply