The House of Favourite Newspapers

Kuvimba kizazi (Adenomyosis)

0

maumivuHii ni hali ambayo huendana na kizazi kuvimba au kujaa husababishwa na tabaka la ndani la kizazi kuzama katika tabaka la kati.

Hapa ieleweke kwamba, kizazi kina tabaka tatu; tabaka la ndani, tabaka la kati na tabaka la nje. Chembe hai za tabaka la ndani huzama ndani kabisa na husambaa katika sehemu yote ya tabaka hilo la kati na kusababisha hali iitwayo ‘Diffuse Adenomyosis’. Vilevile inaweza kukaa humo na kutengeneza vivimbe vidogo vidogo sana ‘Focal Adenomyosis’.

Kuvimba kizazi (Adenomyosis)Mwanamke mwenye tatizo hili la kuvimba kizazi anaweza kupata aina mojawapo ya tatizo hili aidha “Diffuse Adenomyosis au Focal Adenomyosis’. Lakini zote, dalili zake hulingana na daktari kuzigawanya. Hivyo ili kuangalia jinsi ya kutibu, kutenganisha na kujua ni aina gani hutegemea zaidi vipimo vya maabara.

JINSI TATIZO LINAVYOTOKEA

Mwanamke mwenye tatizo hili anahisi tumbo lake linaongezeka kama mjamzito, akipimwa tumbo huonekana kubwa kama ana mimba ya miezi mitatu, tumbo likipapaswa huwa kubwa laini kama mimba.

Jinsi chembe hai za ‘Endometrium’ zinavyozama kwenye tabaka la kati la kizazi bado sababu halisi haijulikani lakini wanasayansi wanadhania hutokana na udhaifu katika hiyo sehemu ya tabaka la kati.

Chanzo kikuu kikiwa ujauzito uliotangulia; yaani kama mwanamke alikuwa mjamzito na endapo alizaa au mimba ilitoka, kama kuna udhaifu katika misuli ya kizazi basi inaweza kusababisha tabaka hilo la ndani kuzama katika tabaka la kati.

Endapo mwanamke aliwahi kufanyiwa upasuaji wa kizazi aidha kutokana na uzazi au kuondoa uvimbe, basi kwa bahati mbaya hali hii inaweza kumtokea. Kushuka kwa mfumo wa kinga ya mwili kwenye kizazi pia ni mojawapo ya tatizo.

Kutokuwepo kwa ukinzani sawa wa vichocheo vya Estrojeni na Projesterone pia husababisha tatizo hili na udhaifu wa tabaka la kati la kizazi na kusababisha chembe hai kujikita humo.

Tatizo hili la kuvimba kizazi hutokea zaidi na kukua kwa kasi pale mwanamke anapokuwa katika umri wa kuzaa na huisha lenyewe anapofikia ukomo wa uzazi kuanzia umri wa miaka 45. Tatizo hili pia husababishwa na hali isiyo ya kawaida ya mgawanyiko wa chembe hai hizi.

NANI HASA ANAWEZA KUPATA TATIZO HILI?

Uzazi wa muda mrefu na umri hasa kuanzia umri wa kuzaa hadi mwisho wa uzazi ni mojawapo ya sababu kubwa za tatizo hili. Kwa tatizo hili la kuvimba kizazi wanawake waliokwishazaa wana nafasi kubwa ya kulipata kwa asilimia tisini na asilimia themanini kwa wanawake wote wenye umri kati ya miaka 40 na 50.

Kuvimba kizazi huhusiana na matatizo au kasoro katika mfumo wa mwili.

Mfano wa hali hii ni uvimbe unaoota ndani ya kizazi na hali ya tabaka la ndani la kizazi kuwa nje na saratani ya kizazi.

DALILI ZA TATIZO

Mojawapo ni dalili zote tulizoelezea hapo awali, mfano kuvimba kizazi na nyingine ni kutoka damu ukeni bila mpangilio na kwa muda mrefu. Pia maumivu makali wakati wa hedhi  na maumivu wakati wa tendo la ndoa.

Hali hii pia inaweza kusababisha ugumba kwa mwanamke kama hajawahi kuzaa au alishawahi kuzaa sasa anatafuta mtoto mwingine lakini kwa muda mrefu zaidi ya mwaka mmoja.Wengine huharibikiwa na mimba ikiwa bado changa.

MATIBABU NA USHAURI

Tiba itazingatia zaidi uchunguzi lakini mojawapo ni kupunguza maumivu na kuyaondoa kabisa, kupunguza damu inayotoka kwa wingi. Matibabu mengine ni upasuaji.

Ni vizuri uwahi hospitali umwone daktari bingwa wa magonjwa ya akina mama katika hospitali za mikoa ili kuona aina gani ya tiba utapata na kupona kabisa.

 

Leave A Reply