The House of Favourite Newspapers

VIDEO: Lijualikali Asimulia Mengi Yaliyomkuta Jela

0

MBUNGE wa Ulanga kwa tiketi ya Chadema, Peter Lijualikali jana alisimulia mengi yaliyomkuta wakati akitumikia kifungo cha miezi sita jela katika Gereza la Ukonga.

Lijualikali alisema wakati akiwa gerezani alitishiwa na polisi kuuawa sambamba na kushuhudia wafungwa wenzake wakipigwa virungu na polisi hali ambayo amesema siyo sahihi kwa mfungwa kufanyiwa vile.

Akizungumza wakati akichangia bajeti ya Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Lijualikali alisema kuwa, wafungwa wengine wamekuwa wakitenda makosa madogo ili wafungwe kifungo kifupi ambapo baadaye hufanya matukio makubwa yakiwemo ya ujambazi.

Lakini wakiachiwa kwa msamaha wa rais kwa yale makosa yao madogo wanakuwa wamepona na kupitisha makosa makubwa hivyo imekuwa ni kichaka cha wao kutekeleza uhalifu kwa vile wananjua wataachiwa huru.

Mbunge huyo amemshauri waziri mwenye dhamana, Mwigulu Nchemba kuhakikisha anafuatilia suala hilo hasa katika Bodi ya Parole ambayo hasa ndiyo wahusika wakuu wa mambo ya vifungo vya wafungwa magerezani na misamaha.

Aidha Lijualikalia amemtaka waziri atembelee magereza akaongee na wafungwa ili kutambua maisha halisi wanaoishi huko magerezani pamoja na mateso wanayoyapata kwani nao ni binadamu kama wengine.

TAZAMA VIDEO AKISIMULIA

Leave A Reply