The House of Favourite Newspapers

Lil Wayne Kufunguliwa Mashtaka

0

MLINZI wa zamani wa rapa Lil Wayne yupo kwenye mipango ya kumfungulia mashtaka bosi wake huyo wa zamani, kwa mujibu wa #TMZ mlinzi huyo anataka kufungua kesi hiyo baada ya Wayne kumtolea bunduki wakati walipokua na mzozo nyumbani kwake mwezi uliopita.

Kwa ripoti ya zamani Wayne anadaiwa kuingia kwenye ugomvi na mlinzi huyo baada ya kupiga picha nyumba yake na kuzivujisha mitandaoni, jambo ambalo lilisababisha ugomvi huo kutokea.

Mwanzo mlinzi huyo hakutaka kumfungulia mashtaka Wayne na sasa amebadilisha mawazo na bado haijafahamika atamfungulia mashtaka gani msanii huyo, lakini kwa mujibu wa #TMZ, mlinzi huyo sasa anadai kuwa Lil Wayne alimpiga kichwani na usoni.

Leave A Reply