The House of Favourite Newspapers

Lipumba Atangaza Kuwavua Uanachama Wabunge 8 wa CUF

0
Profesa Ibrahim Lipumba.

 

Baraza Kuu la Uongozi la Taifa la Chama cha Wananchi (CUF) limewavua uanachama wabunge wanane wa chama hicho kwa madai ya utovu wa nidhamu, yakiwemo kukisaliti chama hicho.

Mwenyekiti wa CUF, anayetambuliwa na Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa, Profesa Ibrahim Lipumba amesema, baraza pia limewavua uanachama madiwani wawili wa viti maalumu mkoani Dar es Salaam, kwa makosa kama hayo.

Profesa Lipumba ametangaza uamuzi huo leo Jumatatu, Julai 24 wakati wa mkutano na wanahabari uliofanyika makao makuu ya CUF, Buguruni, Dar es Salaam.

“Leo asubuhi tumewasilisha nyaraka  za hatua hizi kwa Spika na Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa kwa hatua zaidi,” amesema Profesa Lipumba.

Amesema wabunge hao wanane ni kati ya 10 walioitwa hivi karibuni na Kamati ya Maadili na Nidhamu kwa mahojiano wakitakiwa kujibu tuhuma zinazowakabili za kukihujumu chama hicho kwa maelezo kuwa walitaka kushirikiana na Chadema kumwondoa yeye madarakani.

 

INSTALL GLOBAL PUBLISHERS APP sasa usipitwe na matukio
PAKUA HAPA==>GLOBAL PUBLISHERS APP

FULL VIDEO; Mapambano Ngumi za Global TV – Ubingwa wa Afrika Mashariki na Kati, Tanzania Bingwa

Leave A Reply