The House of Favourite Newspapers

LIVE KUTOKA MOSHI: MWILI wa Dkt MENGI Wawasili Kilimanjaro

MWILI wa aliyekuwa Mwenyekiti wa Makampuni ya IPP, Dkt. Reginald Meng,i umewasili mkoani Kilimanjaro katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA) na kupokelewa na mamia ya waombolezaji.

Familia ya Dkt. Mengi ikiwa Uwanja wa Ndege (KIA) leo asubuhi, kwa ajili ya kuupokea mwili wa marehemu na kuanza safari ya kwenda nyumbani Machame kwa maziko.

Msafara huo umeongozwa na Mkuu wa Mkoa wa Dar  es Salaam, Paul Makonda, ambaye aliambatana na ndugu na watoto wa marehemu.

Waombolezaji  wakiwa Uwanja wa Ndege wa  KIA kwa ajili ya kuupokea mwili wa Dkt. Mengi.

Aidha, baada ya mwili huo kuwasili utapelekwa nyumbani Machame ambako utazikwa kesho Alhamisi.

Vilio vikitawala katika uwanja hapo. 

Mkuu wa Wilaya ya Hai, Lengai Ole Sebaya (kushoto) akiwaongoza waombolezaji kuupokea mwili.
Wafanyakazi wa vyombo mbalimbali vya habari wakiwa  Moshi nje ya Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Usharika wa Moshi Mjini,  ambapo ibada ya mwisho ya kumuaga arehemu Mengi itafanyika.
Moja ya taswira za Kanisa la KKKT itakapofanyika ibada. 

Gari litakaloupokea mwili wa marehemu Mengi. 

Comments are closed.