The House of Favourite Newspapers

Serikali Yatenga Bil 149 Kutekeleza Bima Kwa Wote – Video

0

MKURUGENZI wa Idara ya Habari Maelezo na Msemaji Mkuu wa Serikali, Gerson Msigwa, leo Agosti 28, 2021 amesema serikali imetenga kiasi cha Sh bilioni 149 kwa ajili ya kuanza kutekeleza mpango wa Bima kwa wote.

 

Msigwa amesema serikali itawasilisha Muswada wa Sheria ya Huduma ya Bima kwa Wote katika Kikao cha Bunge la Septemba mwaka huu na kwamba kiasi kilichotengwa ni cha awali na kitaanza kwa makundi maalumu.

 

“Huduma za mfuko wa bima ya afya zina umuhimu mkubwa katika jamii,” amesema Msigwa wakati wa Mkutano wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) na Wahariri unaofanyika jijini Dodoma kama sehemu ya maadhimisho ya miaka 20 tangu mfuko huo uanzishwe.

Leave A Reply