The House of Favourite Newspapers

Mkuu wa Shule Aonywa Kisa Amber Rutty

0

​​​​​​​UONGOZI wa Halmashauri ya Manispaa ya Temeke umeonesha kuchukizwa na kitendo cha Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Nzasa cha kumualika Amber Rutty kuwa kama mgeni rasmi na kuongea na Wanafunzi.

 

“Kumekua na taarifa zinazosambaa kupitia kipande cha video mitandaoni zikimuonesha mtu mmoja akitembelea Shule ya Msingi Nzasa iliyopo Temeke, akiwa amevaa mavazi yaliyo kinyume na maadili ya Kitanzania….”

 

“Tunapenda kutoa taarifa kwamba uongozi wa manispaa ya Temeke umechukizwa na ugeni huo pia hauhusiki kwa namna yoyote juu ya mualiko wa mgeni huyo”

 

“Aidha uongozi wa Manispaa ya Temeke umemuonya Mkuu wa shule kwa kukiuka maadili ya utumishi wa umma kutokana na kitendo kilichotokea, uongozi unaomba radhi kwa usumbufu wote uliojitokeza,” kimesema Kitengo cha Habari na Uhusiano, Manispaa ya Temeke.

 

Leave A Reply