The House of Favourite Newspapers

Video: Polepole Aongoza TAMASHA la Nguvu za Mwanamke

0

Bajeti ya Sekta ya Afya nchini Tanzania imeweza kupanda kutoka Billioni 30 hadi Billioni 271 kutokana na uwepo wa watendaji wazuri waliopewa dhamana ya kumsaidia Rais kwenye kiutendaji.

 

Hayo yamesemwa leo Agosti 2, 2020 na Katibu wa Itikadi na Uenezi wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Humphrey Polepole katika Tamasha la Nguvu ya Mwanamke katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam, ambapo ameeleza tangu kuteuliwa kwa Dkt. Zainabu Chaula kuwa Naibu Katibu Mkuu TAMISEMI kumekuwa na mabadiliko chanya katika sekta ya afya.

 

“Mwaka 2013 hadi 2014 bajeti ya afya, dawa, vifaa tiba, na kadhalika ilikuwa Billioni 30 baada ya daktari Bingwa Zainabu Chaula kuingia 2016-2017, 2017-2018, 2018-2019 wakatoka Billioni 30 hadi Bilioni 269, Bilioni 270 na sasa Bilioni 271”, ameeleza.

 

Aidha Polepole amesema kuwa uwepo wa Dkt. Zainabu pamoja na watendaji wenzake waliopo TAMISEMI ndio umechangia katika kuleta mabadiliko hayo katika sekta ya afya huku akiongeza kuwa upatikanaji wa dawa katika vituo vya afya hivi sasa ni asilimia 90.

 

Polepole ni muongozoja katika Tamasha hilo lililobeba lengo la kuonyesha mafanikio yaliyopatikana kupitia changamoto mbalimbali na kuwafanya wanawake wengine kutumia changamoto kama fursa.

 

Leave A Reply