The House of Favourite Newspapers

VIDEO: Rais Magufuli Azindua Stendi Mpya ya Mabasi Korogwe -Tanga

0
Stendi Mpya ya Mabasi wilayani Korogwe.

 

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, John Pombe Magufuli amezindua rasmi stendi ya mabasi wilayani Korogwe, Tanga akihitimisha ziara yake ya siku tano mkoani humo.

Katika shughuli ya uzinduzi huo uliohudhuriwa na mamia ya wananchi wa Korogwe na viongozi wa ngazi mbalimbali serikali, Rais Magufuli amerudia kuwaelezea wananchi wake mafanikio yaliyopatikana tangu aingie madarakani, ikiwa ni pamoja na kufufuliwa kwa shirika la ndege na kununua ndege kadhaa mpya.
Mradi wa reli ya kiwango cha ‘standard gauge’ na kutumbua majibu, ni miongoni mwa mambo ambayo Rais Magufuli amesema yamefanywa kikamilifu na serikali yake, kwa lengo la kuwasaidia wananchi kuboresha maisha yao.

Pia amewakumbusha wananchi juu ya umuhimu wa kufanya kazi kwa kujituma na kueleza kwamba yeyote ambaye atalegalega kufanya kazi, hata hizo fedha kidogo alizonazo zitapotea wakati wachapakazi wakineemeka.

Pia amesema kwa mwaka huu wa serikali, ajira zaidi ya 50,000 za kada mbalimbali, zitatolewa huku akiahidi kushughulikia matatizo ya wananchi wake hasa wafanyakazi, yakiwemo ya kuchelewa kupandishwa madaraja kazini.

Wengine waliopata fursa ya kuzungumza kwenye uzinduzi huo, nio Mbunge wa Korogwe Vijijini, Steven Ngonyani “Maji Marefu’, Ummy Mwalimu, na wengineo.

Leave A Reply