The House of Favourite Newspapers

LIVE: Rais Magufuli Apokea Nyumba 50 za Mkapa Foundation -Chato

0

Rais mstaafu wa awamu ya tatu, Benjamin Mkapa ametembelea na kuzindua nyumba ya wahudumu wa afya katika kijiji cha Mkungo wilayani Chato mkoani Geita zilizojengwa na taasisi ya Mkapa Foundation kwa kushirikiana na Serikali.
 
Rais Magufuli akisalimiana na Rais Mstaafu, Benjamin Mkapa
Akizindua nyumba hizo jana, Rais Mkapa aliwasalimia wanachi kwa salam yake ya “mambo” na wananchi kuitika poa” na kuwataka kutunza nyumba hizo na kushirikiana vema na watumishi watakaoshi katika nyumba hizo kisha msafara wake kuondoka na kuelekea Ikulu ndogo iliyopo Chato.
Rais Magufuli akisalimiana na Balozi wa Japan nchini Tanzania, Masaharn Yoshida.
Mkapa aliingia katika eneo la zahanati hiyo saa sita mchana akiongozana na mkewe, Mama Anna Mkapa na Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu.

 

Uzinduzi wa nyumba hiyo ni ishara ya kuzindua nyumba nyingine 50 zilizopo katika mikoa ya Geita, Simuyu na Kagera .
 
Makabidhiano ya nyumba hizo yanatarajiwa kufanyika leo(Jumatatu July 10)  katika uwanja wa mpira wa miguu uliopo Chato mjini hafla itakayohudhuriwa na Rais John Magufuli.
Rais Magufuli akimpokea na Rais Mstaafu, Benjamin Mkapa
Ofisa Mahusiano na Mawasiliano wa Mkapa Foundation, Deogratius Rimoy alisema nyumba 50 zilizojengwa na taasisi hiyo katika mikoa mitatu tofauti zimegharimu kiasi cha Sh 2.5 bilion
Alisema lengo la kujenga nyumba hizo ni ili kuboresha huduma za afya vijijini illi watumishi waweze kutoa huduma za afya kwa saa 24.
Leave A Reply