The House of Favourite Newspapers

Video: Rais Samia na Kenyatta Wafungua Kongamano la Wafanyabiashara

0

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan na Rais wa Jamhuri ya Kenya Mhe. Uhuru Kenyatta washiriki kongamano la wafanyabiashara (#Kenya#Tanzania high level business forum) katika ukumbi wa Serena Hotel Nairobi – Kenya.

Tanzania na Kenya zimefungua ukurasa mpya katika kuimarisha uhusiano na ushirikiano baada ya kukubaliana kutekeleza kwa pamoja mambo matano muhimu.

 

Makubaliano hayo yalifikiwa jana jijini Nairobi, Kenya kufuatia ziara ya siku mbili ya Rais Samia Suluhu Hassan iliyoanza jana katika nchi hiyo kwa mwaliko wa Rais Uhuru Kenyatta.

 

MAKUBALIANO MATANO

  1. Kuimarisha tume ya ushirikiano
  2. Kuimarisha sekta ya mawasiliano
  3. Ujenzi bomba la gesi kutoka Dar hadi Mombasa
  4. Kuimarisha usalama baina ya nchi mbili
  5. Kuimarisha utamaduni na masuala ya kijamii Katika mawasiliano.
Leave A Reply