The House of Favourite Newspapers

Darassa Avunja, Ukimya Aibuka Upya – Video

0

 

RAPA maarufu Bongo, Darassa, amesema watu wengi walikuwa wakim-dis kwamba yupo kimya kwa sababu zao binafsi lakini ukweli ni kwamba alikuwa chimbo akiandaa bonge la albamu ambayo kwa sasa inatikisa Bongo nzima.

 

Darassa amesema hayo leo Alhamisi, Janauari 7, 2020, wakati akifanya mahojiano na Kipindi cha Bongo 255 cha +255 cha Global Radio wakati akitambulisha albamu yake mpya aliyoipa jina la ‘A SLAVE BECOMES A KING’.

 

“Nimeamua kuiita albamu yangu ‘Slave Becomes a King’ kwa sababu tunataka kuleta mabadiliko flani ya kifikra kwenye jamii, hatuwezi kuwa ng’ombe wa maskini siku zote, lazima tufanye vitu ambavyo ipo siku tutaheshimika,” alisema.

 

“Mimi huwa sipendi kufanya vitu vyepesi, napenda kufanya vitu ambavyo vitakuwa vya tofauti, ndivyo nilivyozoea. Studio yoyote ninayoenda kufanya nayo kazi lazima utakuta mafaili yangu ya muziki.

“Sitaki kuona washkaji zangu wanakaba, wanaiba mtaani, sitaki kuona watu wanakuwa wanyonge ama wanalia, lazima tu-fight, haya ni maisha siYo kila siku tunaimba ngoma za huzuni, sipendi kutia huruma, lazima tufurahie pia,” amesema Darassa.

TAZAMA FULL VIDEO

Leave A Reply