The House of Favourite Newspapers

Lulu Diva: Sitaki Tena Mambo ya Mkorogo

0

LULU Abbas ndilo jina halisi alilopewa na wazazi wake. Lakini jina la kutafutia tonge la kila siku kupitia uimbaji alijipachika jina la Lulu Diva.

Huyu ni mtoto pekee kwa baba na mama yake ambaye kwa hivi sasa anapitia changamoto ya kuumwa takriban miaka mitano kitandani huku baba yake mzazi akiwa ametangulia mbele ya haki.

 

Gazeti la Ijumaa limezungumza naye jambo kubwa la muonekano wake wa tofauti kwa sasa na alivyokuwa siku za nyuma.

Hivi sasa Lulu Diva anaonekana amekuwa na rangi nyeusi ambayo alikuwa nayo awali, laikini ikapotea, IJUMAA limezungumza naye mambo mengi kama ifuatavyo;

 

IJUMAA: Mambo vipi Lulu Diva?

LULU DIVA: Poa, leta habari…

IJUMAA: Hongera sana, naona unazidi kukomaa kwenye gemu na hujakata tamaa.

 

LULU DIVA: Ni Mungu tu maana hata ukikata tamaa utakula wapi, nakomaa tu mpaka kieleweke na ninakomaa hasa mtu akiniona kwenye steji anaweza asinielewe, lakini ukweli ndiyo ninapopatia riziki yangu ya kila siku.

IJUMAA: Ni muda mrefu sana hujaweka wazi masuala yako ya kimapenzi, ni kwa nini au upo singo?

 

LULU DIVA: Sipo singo, lakini nimeacha kuweka hadharani uhusiano wangu kwa sababu zangu binafsi maana kama mpenzi ni wa kwangu kwa nini wengine wamjue, wanapata faida gani sasa, wakati mwingine tuweke mambo yetu chumbani na tusiyatoe hadharani kwa sababu hayana faida zaidi ya kuwaumiza wengine.

IJUMAA: Vipi kuhusu afya ya mama yako anaendeleaje?

 

LULU DIVA: Kwa kweli kila kukicha tunashukuru sana Mungu.

IJUMAA: Nani anabaki naye nyumbani unapokuwa misele?

LULU DIVA: Kuna watu na hata mimi nikitoka ni kwa ajili ya kutafuta kwa sababu yake, maana hakuna kitu ninachoniumiza kama kumuona mama yangu yupo kitandani anaumwa siku zote, anateseka, huwa ninakaa na kulia mno, lakini nasema yupo Mungu, siku moja muweza wa yote atamponya.

 

IJUMAA: Lulu Diva unaonekana tofauti sana kwenye muonekano tofauti wa ngozi yako nini kimefanyika?

LULU DIVA: Kwa kweli nilitumia kitu kikaniaharibu sana ngozi yangu; yaani hata kutoka nilikuwa naona aibu sana, lakini mtu akanishauri niende sehemu ambapo walinisafisha makovu yangu yote na kuirudisha ngozi yangu na ndiyo maana niko tofauti na sitaki tena mambo ya mkorogo kabisa, nabaki na ngozi yangu.

 

IJUMAA: Hongera sana kwa sababu naona kama umekuwa mweusi tofauti na zamani.

LULU DIVA: Asante sana.

IJUMAA: Vipi kuhusu kupata mtoto au unataka uwe mtu mzima ndipo uitwe mama?

LULU DIVA: Mungu akipenda mbona ni haraka tu kwa sababu kuitwa mama ni jambo jema; tena mimi nataka watoto wengi sana, waje wanisaidie baadaye kwa sababu mimi nimezaliwa peke yangu, najiona hapa ninavyoangaika na mama yangu.

 

IJUMAA: Haya nakushukuru sana Lulu Diva kwa ushirikiano wako.

LULU DIVA: Asante sana, nawapenda mashabiki wangu wanaosoma Gazeti la IJUMAA.

MAKALA; IMELDA MTEMA, BONGO

Leave A Reply