The House of Favourite Newspapers

Maalim Azungumzia Corona, Madeni Nchi Changa Yasimamishwe – Video

0

MWENYEKITI  wa ACT-Wazalendo, Maalim Seif Sharrif Hamad, leo Aprili 4, 2020,  ametoa rai kwa Watanzania kuchukua tahadhari zote dhidi ya ugonjwa wa Covid-19 unaoambukizwa na virusi vya Corona, na amezitaka nchi zilizoendelea kusimamisha kwa mwaka mmoja madeni dhidi ya nchi zinazoendelea ili kuzipa nchi hizo nafasi ya kujenga mfumo bora wa huduma za afya

 

Ameyasema hayo katika mkutano na waandishi wa habari katika ofisi za chama hicho huko Zanzibar ambapo amewataka wakazi wa visiwa hivyo kuwa walinzi dhidi ya watu kutoka nje ili  kuzuia maambukizo ya virusi hivyo hatari.

 

“Kwa namna ya pekee, naomba nizungumze maneno haya na wanafunzi wetu, kwa maana ya vijana wetu na watoto wetu wanaosoma ambao kwa sasa mko majumbani kutokana na skuli, taasisi za elimu ya juu na vyuo vikuu kulazimika kufungwa ili kuepusha uwezekano wa maambukizo ya virus vya corona,” alisisitiza.
Kuhusiana na ushiriki wa kimataifa katika kupiga vita janga la ugonjwa huo, Maalim alisema nchi tajiri, pamoja na kukumbwa pia na janga hilo zinaweza  kusaidia kwa kusimamisha madeni kwa nchi changa ambazo nazo zinakabiliwa na tatizo hilo.
“Ninatumia nafasi hii kuiomba jamii ya kimataifa na hasa mashirika na taasisi za fedha duniani kusaidia nchi zinazoendelea kwa kusimamisha kwa mwaka mmoja malipo ya madeni ili kutumia fedha zinazookolewa kujenga mfumo wa afya utakaoweza kusaidia watu masikini,” alisema.

Leave A Reply