The House of Favourite Newspapers

Mabondia wa Ndondi za Global TV Watambulishwa Rasmi, Jumapili Kazi Ipo!

0
Kutoka kushoto ni Meneja wa Kamwamba, Craig Roussean, mabondia Israel Kamwamba, Regin Champion na Yohana Banda.

 

JUMLA ya mabondia sita wanaotarajia kupanda ulingoni keshokutwa kushindania ubingwa Global TV, Afrika Mashariki na Kati leo wametambulishwa kwa waandishi wa habari katika mkutano ulifanyika Hoteli  ya The Atriums iliyopo Sinza- Afrika Sana, Dar.

 

Rais wa TPBO, Yasin Abdallah ‘Ustadh’ (katikati) akiwatambulisha mabondia hao (hawapo pichani) kwa wanahabari.

Mapambano hayo ya ubingwa yatapigwa kwenye Ukumbi wa Dar Live, uliopo Mbagala Zakhem na kurushwa mubashara na kituo cha Global TV Online kupitia website yake ya www.globaltvtz.com huku yakiambatana na burudani ya muziki  kutoka kwa wasanii wakali wa Bongo Fleva.

 

Mratibu wa Global TV, Juma Mbizo akizungumza na wanahabari.

Katika utambulisho huo Rais wa Kamisheni ya Ngumi za Kulipwa Tanzania (TPBO), Yassin Abdallah ‘Ustaadh’ alisema kuwa kufuatia kupokea maombi ya wadau wengi wameamua kuweka kiingilio cha shilingi 5,000 kwa watu wa kawaida na VIP shilingi 20,000 tu.

 

Wanahabari wakifuatilia tukio hilo.

Ustaadh ameongeza kuwa pambano hilo litarushwa live na Global TV hivyo amewataka wadau kuendelee kujiunga kwenye mtandao wa channel hiyo ili kushuhudia pambapano hilo la kihistoria.

Craig Roussean akizungumza na wanahabari.

Katika hatua nyingine, pambano hilo, mashabiki wataweza kulishuhudia mubashara kupitia simu zao za mkononi kwani litaoneshwa na Global TV pekee. Wadau na mashabiki watakaopata nafasi ya kuingia ukumbini wataingia kwa kadi maalum za mwaliko.

Israel Kamwamba wa malawi akizungumza na wanahabri.

Ili kulishuhudia pambano hilo kwa njia ya simu tena bure, hakikisha unajiunga (SUBSCRIBE) na YouTube Channel ya Global TV Online sasa hivi ili usipitwe. Ingia YouTube, tafuta GLOBAL TV ONLINE, kisha bonyeza neno SUBSCRIBE pia bonyeza kikengele kidogo kilichopo pembeni yake ambacho kitakukumbusha kuangalia pambano hilo mara tu litakapoanza.

Nasibu Ramadhan ‘Pacman’ akizungumza na wanahabari.

Kama wewe umeshajiunga, basi hakikisha pia umebonyeza kikengele ili usipitwe na kila kinachoendelea Global TV. Pia unaweza kutupata kupitia mtandao wa www.globaltvtz. com, jiunge sasa na Global TV ili uwe wa kwanza kuona ndondi za kimataifa. Kajiunge sasa kwa kuingia www.youtube.com/user/ uwazii.

Yohana Banda akijinadi.

 

Bondia Idd Pialali wa Tanzania akizungumza na wanahabari.

 

Regin Champion wa Congo akizungumza na wanahabari.

 

PICHA NA RICHARD BUKOS, STORI NA IBRAHIM MUSSA | GLOBAL TV

Leave A Reply