The House of Favourite Newspapers

Madai ya Kuiacha Familia na Kuishi Hotelini, OFM Yamfungia Kazi Gabo

gabo_0Stori: Waandishi Wetu |AMANI

DAR ES SALAAM: Kufuatia madai ya staa anayetamba Bongo kwa sasa, Salim Ahmed Salim ‘Gabo’ kwamba ameiacha familia yake na kwenda kuishi hotelini akila bata, kikosi cha Oparesheni Fichua Maovu (OFM) cha Global Publishers kimemfungia kazi nyota huyo ili kubaini ukweli, sikia ilivyokuwa!

Ubuyu kuhusu mkali huyo mwenye mvuto kwenye kioo kulowea hotelini akila raha ulitolewa na chanzo chetu cha kuaminika ambacho ni mmoja wa watu wa karibu wa staa huyo (jina tunalo) ambapo alisema kuwa, tabia hiyo yeye mwenyewe inamchukiza kwa sababu Gabo ni mtu mwenye familia.gabo-2

Gabo akiingia hotelini hapo.

“Unajua jamaa kaiacha familia yake kule Mbagala, leo anaishi kiwanja hiki kesho hiki, yaani kabadilika, si kama zamani. Wakati mwingine huwa najiuliza anakuwa anashuti filamu huko au, lakini si bure,” kilisema  chanzo chetu.

Hata hivyo, Amani lilimbana sosi kufafanua vizuri zaidi juu ya Gabo kuishi hotelini maana isije kuwa yupo kambini akishuti muvi, lakini alisisitiza kuwa, mapaparazi wafanye uchunguzi wao na watabaini ukweli wote.

gabo-3

OFM MZIGONI

Baada ya kuupata ubuyu huo na kuuweka mbele ya dawati lake, kikosi cha OFM kilianza mara moja kufanyia kazi madai hayo kwa kufanya uchunguzi.

Kazi ilianza kwa OFM kuchunguza kupitia kwa masnichi wake wazuriwazuri ni wapi jamaa huyo alikuwa anaishi wakati huo, ndipo iliponasa kuwa, alikuwa amejichimbia kwenye hoteli moja iliyopo Magomeni ya Mwembechai.

gabo-5

Gabo akiwa na jamaa yake.

OFM HOTELINI

Mara moja kikosi hicho kiliamua kutia timu mpaka kwenye hoteli hiyo iliyosemekana kuwa staa huyo ambaye hivi karibuni alijizolea tuzo mbili za EATV ambazo ni Tuzo ya Muigizaji Bora wa Kiume na Tuzo ya Filamu Bora ya Mwaka, alikuwa akiishi.

Baada ya kufika hotelini hapo asubuhi na mapema na kupiga kambi, baadaye OFM ilimshuhudia msanii huyo akitembeatembea katika mazingira ya hoteli hiyo utadhani nyumbani kwake, maana alikwenda kwenye mgahawa kupata kifungua kinywa na baadaye akaenda kwenye bustani ya hoteli hiyo na kuweka pozi akipiga stori na baadhi ya watu waliokuwepo bustanini hapo.

OFM iliendelea kumfuatilia ambapo baadaye aliondoka hotelini hapo, lakini kwa uchunguzi wa OFM hata siku iliyofuata Gabo alikuwepo hotelini hapo akiendelea na maisha yake ya kula bata kama kawaida.

gabo-4

GABO ATAFUTWA

Baada ya makachero wa OFM kumnasa kiulaini staa huyo waliamua kumvutia waya ili aweze kufungukia madai hayo, lakini alipopokea simu na kusomewa mashitaka yake alianza kuwaka:

“Mi sizijui hizo habari bwana, mbona kwenye mambo mengine huwa hamnitafuti, mkisikia masuala ambayo si ya maana ndiyo mnanitafuta, acheni mambo yenu (akakata simu).

gabo-1

SIKIA WE GABO

Lengo la OFM ilikuwa ni ‘kubalansi’ madai ambayo ilikuwa imeyapata na kuyathibitisha kwa picha, lakini badala yake Gabo aliwaka na kukata simu huku akishutumu kuwa Global Publishers huwa haimtafuti kwa mazuri  mpaka anapokuwa na skendo.

Hata hivyo, wakati anatafutwa kubalansi stori hiyo ilikuwa ni muda mfupi tu alipotoka kuchukua Tuzo za EATV, ambapo aliandikwa na kupongezwa lakini pia alitafutwa kwa ajili ya makala na akadai kuwa alikuwa ‘bize.’

Mbali na hapo, Gabo amekuwa akitafutwa mara kwa mara na wahariri wa Global Publishers kwa ajili ya kufanyiwa makala na stori lakini amekuwa akitoa udhuru na kuonekana yupo bize na mambo yake, hana ushirikiano lakini madai yake ni kwamba hatafutwi!

Miongoni mwa udhuru ni pale alipopigiwa simu na kusema: “Nipo mikoani kaka, nikirudi Dar nitakwambia.” Hata hivyo, hakuwahi kusema amerudi licha ya kunaswa hotelini.

Shinda Nyumba Awamu ya Pili Yatikisa Jiji la Dar es Salaam

Comments are closed.