The House of Favourite Newspapers

Madaktari Wamvaa Wolper Kisa Ulevi Akinyonyesha

0

 

WANASEMA siku zote kuzaa siyo kazi, bali kazi ni kulea na hicho ndicho kinachojiri kwa supastaa wa Bongo Movies, Jacqueline Wolper Massawe ambaye amezua gumzo kila kona baada ya kudai kuwa, pombe inamsaidia kupata maziwa ya kumnyonyesha mwanawe P aliyezaa na mwanamitindo Rich Mitindo.


Hata hivyo, madaktari
mbalimbali waliozungumza na Gazeti la IJUMAA wamemvaa mwanamama huyo kwa kueleza madhara makubwa ya mama anayenyonyesha kuendelekeza ulevi.

 

Kupitia ukurasa wake wa Snapchat, Wolper au Mama P ameweka picha ya bia aliyokuwa anakunywa na kuandika; “Jamani P jamani, bia chungu, mnawezaje wenzangu uuwiii…Nimeambiwa inaleta maziwa, anything for P pliiiz…

 

Madaktari hao wamesema kuwa, kwa kawaida mama hutakiwa kumnyonyesha mtoto wake kuanzia kipindi cha mwaka sifuri hadi miezi sita bila kumpatia chakula au kinywaji cha aina yoyote.

 

Kwa mujibu wa daktari maarufu jijini Dar, Dk Abdallah Mandai, mama anayenyonyesha huku akiwa ametumia kilevi anamuweka mtoto wake kwenye hatari ya kuathirika afya ya ubongo na kupata tatizo la utindio wa ubongo.

 

“Kumbuka, mtoto hutegemea kula na kunywa kila kitu kutoka kwa mama yake hivyo mama akinywa pombe huwenda moja kwa moja kwa mtoto naye huipokea na kuinywa.

 

“Unywaji pombe ni hatari kwa mama anayenyonyesha na haruhusiwi kutumia kilevi cha aina yoyote, pombe huathiri afya ya mtoto, kuna uwezekano mkubwa mtoto akawa na hitilafu kuanzia mfumo wa fahamu, uzito mdogo, kichwa kidogo na madhara mengine mengi,” anabainisha.

 

“Mtoto huyo kama mama yake ni mlevi, basi hunywa pombe kupitia maziwa ya mama yake hivyo kumuathirika,” anasema na kuongeza;

 

“Wanawake wajue kwamba unapotumia kilevi cha aina yoyote ile, kilevi hicho huenda hadi kwenye maziwa yake na mtoto hupokea kilevi hicho kupitia maziwa ya mama yake pindi anaponyonya, ni hatari kwa afya yake.

 

“Wapo wanaofikiri kwamba madhara hujitokeza wakati wa ujauzito pekee na wanapojifungua hawajali wakati wa kunyonyesha wanaendelea kutumia vilevi, wanalewa tu, jambo ambalo ni hatari kwa afya ya mtoto.”

 

Anasema ni hatari kwa mama anayenyonyesha kutumia vilevi kwani humuathiri mtoto wake kwa namna moja au nyingine. Daktari huyo anasema mama anapolewa na kumnyonyesha mtoto wake, mtoto huyo naye hulewa kwani hupata kilevi kupitia maziwa ya mama yake.

 

“Ile pombe anayokuwa amekunywa mama huwenda kwenye maziwa yake, mtoto huipokea pindi tu anaponyonya, ni hatua mbaya mno na ni hatari kwa afya ya mtoto husika kwa sababu kilevi kile huwenda kuathiri afya ya ubongo wake,” anasema.

 

Daktari huyo anasema madhara yake ni kwamba mtoto husika huwa kwenye hatari kubwa ya kupata tatizo hilo la utindio wa ubongo katika maisha yake.

 

Anamalizia kuwa, pamoja na kuathiri maziwa ya mama, vilevi vina athari nyingine nyingi kwa watumiaji wa jinsi zote mbili

Leave A Reply