The House of Favourite Newspapers

Magufuli Atoa Siku 14 Vituo vya Mafuta Kutumia EFDs

0
Rais Dkt. John Magufuli akipeana mkono na Waziri wa Ujenzi, Prof. Makame Mbarawa baada ya kuzindua barabara hiyo.
 
Rais John Magufuli ametoa siku 14 kwa wamiliki wa vituo vya mafuta kote nchini kutumia mashine stahiki za risiti za kielektroniki (EFDs) huku akisisitiza kuwa watakaoshindwa watafutiwa leseni zao.
Hayo ameyasema leo mjini Biharamulo wakati akizindua Barabara ya Kagoma – Biharamulo – Lusahunga.
 
Rais Magufuli akisalimiana na wananchi wa Biharamulo.
 
Hivi karibuni, Waziri wa Fedha na Mipango, Prof. Philip  Mpango alivifungia baadhi ya vituo vya mafuta hapa nchini baada ya kubainika kuwa vilikuwa havitumii mashine stahiki za EFDs kinyume cha sheria jambo ambalo linaifanya serikali kukosa mapato yake kulingana na mauzo ya mafuta hayo.
 
Wakati huohuo, Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa amesema Barabara ya Kagoma – Biharamulo – Lusahunga imegharimu Sh 190 bilioni.
 
Rais akiwapungia mkono wananchi wa Biharamulo.
 
Mbarawa ametoa tamko hilo leo wakati akiizindua mbele ya umati mkubwa wa watu ambao walihudhuria uzinduzi wa barabara hiyo ya kiwango cha lami yenye urefu wa kilometa 154.
 

Katika hatua nyingine, akizindua ujenzi wa barabara hiyo, Rais John Magufuli amesema pia kwamba, Biharamulo imeshika nafasi ya pili kwa umaskini na wananchi wanafanya ulinganisho na hali ilivyo tofauti katika wilaya jirani ya Chato.

 
Rais akisalimiana na wazee wa Biharamulo.
 
Kwa upande wake Mbunge wa Biharamulo, Oscar Mukasa amesema wanaunga mkono msimamo wa Rais kupiga marufuku wanafunzi wanaobeba mimba kuendelea na masomo na wameanzisha shule ya wasichana ya bweni kuunga mkono kauli yake.
Leave A Reply