The House of Favourite Newspapers

Mahaba ya Diamond na Zari Usipime, Barnaba Atoa Ombi Zito kwa Mastaa Hao

0
Zari mama wa Tiffah aliyezaa na Staa wa Muziki wa Afrika kutoka Tanzania Diamond Platnumz

TIFFAH DANGOTE; ni mmoja wa watoto wawili wa staa wa muziki barani Afrika, Diamond Platnumz aliyezaa na mwanamama tajiri, Zari The Boss Lady ambaye Jumamosi Agosti 6, 2022 alikuwa akitimiza umri wa miaka 7; mtoto wao mwingine ni Prince Nillan.

 

Shughuli ya kukata na shoka ilifanyika nchini Afrika Kusini na kuhudhuriwa na ndugu, jamaa na marafiki wa familia ya Diamond na ile ya Zari.

Tiffah ametimiza umri wa miaka 7

Kubwa kuliko ni kusambaa kwa video ambazo zinaonesha mahaba mazito baina ya Diamond na Zari ambao ni ma-ex wanaopendwa zaidi.

 

Katikati ya mahaba hayo, mmoja wa waalikwa alikuwa msanii Barnaba Classic ambaye amemuomba Zari chondechonde arudiane na Diamond.

Diamond Platnumz

Video nyingi zinamuonesha Zari akideka kifuani mwa Diamond huku akiwa na furaha kama yote na kicheko hakikauki bila kusahau kivazi hadimu mno na chepesiii ambacho Mama Tee alimvalia Baba Tee.

 

Na habari za ndani tulizoamka nazo leo ni madai mazito kwamba, huwenda walipasha kiporo!

Cc; @sifaelpaul.

 

Leave A Reply