The House of Favourite Newspapers

Mahaba ya Wema Rubani Mubashara

0

Miongoni mwa mambo yanayozua mjadala mkali ni mahaba ya mwanadada Wema Sepetu na Rubani Danzack ambayo sasa ni mubashara.

Stori ya wawili hao kuwa huwenda wapo kwenye mapenzi ni ya muda mreu.

Kama utakumbuka kuna wakati Danzack alidai kuwa yupo tayari kupeleka mahari nyumbani kwa wazazi wa Wema.

Katika moja ya video za juzikati, Wema alimualika Danzack kwenye kipindi chake cha Cook With Wema ambapo walipata fursa ya kuoneshana mahaba ya kufa mtu huku wakishirikiana kupika na kula huku mazungumzo yote yakitawaliwa na mahaba; si unajua ile sauti ya Wema?

Katika maelezo yake, Wema anamsifia jamaa huyo kuwa anajua jinsi ya kumfanya mwanamke ajione wa pekee na amemfanya apagawe.

Cc; @sifaelpaul

Leave A Reply