The House of Favourite Newspapers

Majaliwa: Kutangaza Nyongeza ya Mishahara Kunaongeza Gharama za Maisha

0

WAZIRI mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Kassim Majaliwa amesema kutangaza nyongeza ya mishahara ya wafanyakazi hadharani hakuna tija kwani kunaongeza gharama za maisha.

 

 

Mtendaji mkuu huyo wa shughuli za Serikali ametoa kauli hiyo bungeni mjini Dodoma leo Alhamisi Februari 11, 2021 katika kipindi cha maswali ya papo kwa hapo na kubainisha kuwa nia ya Serikali ni kuendelea kuboresha maslahi ya wafanyakazi nchini.

 

 

Alikuwa akijibu swali la mbunge wa Konde (ACT-Wazalendo), Khatibu Said Haji aliyehoji ni lini Serikali itaboresha maslahi ya wafanyakazi nchini ikiwemo kupandishiwa na kuboreshewa maslahi.

 

 

Majaliwa amesema Serikali ilipoingia madarakani ilibaini kuwa kutangaza hadharani mishahara ya watumishi ni kuongeza gharama za maisha.

 

 

“”Serikali ya Awamu ya 5 ilijifunza tukitangaza hadharani kupandisha mishahara vitu vingi vinapanda bei, kupandisha mshahara wa elfu 20 au 30 haina tija, natoa wito watumishi wa Umma wasikate tamaa wakidhani kutangaza mishahara Hadharani ndiyo kunaweza kutatua matatizo,” amesema Majaliwa.

 

Leave A Reply