Makamu wa Rais Dkt Philipo Mpango Azindua kituo cha afya Ketumbeine Loliondo mkoani Arusha
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt Philipo Mpango leo Februari 10, 2024 amezindua kituo cha afya Ketumbeine kilichopo Wilaya ya Loliondo mkoani Arusha ambacho kimegharimu kiasi cha Shilingi Bilioni 1.32. Utoaji wa huduma za afya katika kituo hicho kitakuwa ni msaada mkubwa kwa wananchi kupata huduma bora za afya karibu na maeneo yao, Kituo hicho kitahudumia vijiji vinne katika Wilaya hiyo.