The House of Favourite Newspapers

Makeke Ujio Mpya wa Queen Darleen

0

MEGASTAA wa muziki barani Afrika, Nasibu Abdul almaarufu Diamond Platnumz ambaye pia ni Mkurugenzi wa Lebo ya Wasafii Classic Baby (WCB), ameweka wazi makeke ya ujio mpya wa first lady wa WCB, Mwanahawa Abdul au ‘Queen Darleen.

Kupitia Insta Story yake, Diamond amethibitisha ujio huo kwa kushea video fupi ikimuonesha Darleen akiwa studio tayari kwa ajili ya maandalizi ya kazi mpya.

Kwa muda mrefu, Darleen amekuwa kipya akijihusisha zaidi na masuala ya kifamilia ambapo aliingia kwenye ndoa na kujaaliwa mtoto hivyo akawa kwenye likizo ya uzazi, lakini uongozi wake umeeleza juu ya ujio wake mpya kwa mwaka huu wa 2022.

STORI; KHADIJA BAKARI, DAR

Leave A Reply