The House of Favourite Newspapers

Malaika Atumia Mamilioni kwa Ishu Hii!

0

SEXY lady wa Bongo Fleva, Diana Exavery ‘Malaika’ amesema ametumia mamilioni kwenye ‘teeth braces’ (urembo wa meno) ili kuongeza mvuto wa tabasamu lake.

 

Mrembo huyo aliyetamba na ngoma kama Rarua amesema vyumavyuma hivyo alivyoweka kwenye meno yake vimemgharimu zaidi ya shilingi milioni nne za Kitanzania na aliwekea nchini Marekani.

 

Kwa sasa Malaika anafanya vizuri na wimbo wake mpya unaokwenda kwa jina la Baila mara baada ya ukimya wa muda mrefu.

 

Ukiachana na ya Malaika, utakumbuka Oktoba, 2017 kwenye sherehe ya 40 ya mtoto wa mwanamitindo Hamisa Mobeto, msanii Gift Stanford ‘Gigy Money’ alidai kuwa nywele alizokuwa nazo usiku huo zilimgharimu shilingi milioni sita!

STORI: IMELDA MTEMA, DAR

Leave A Reply