The House of Favourite Newspapers

Mama Dangote Ampigia Saluti Zari

0

MAMA mzaa chema wa staa mkubwa wa muziki barani Afrika kutoka nchini Tanzania, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’, Sanura Kassim ‘Mama Dangote’, amempigia saluti mmoja wa wakwe zake, Zarinah Hassan ‘Zari The Boss Lady’.

 

Mama Dangote anasema kuwa, katika wakwe zake wote, mkwe ambaye yuko ndani ya moyo wake siku zote ni mwanamama Zari, mwenye maskani yake kwa Madiba nchini Afrika Kusini.

 

 

Zari amemzalia Mama Dangote wajukuu wawili, Tiffah Dangote na Prince Nillan ambao Zari amezaa na Diamond au Mondi.

 

 

Wengine waliozaa na Mondi ni mwanamitindo Hamisa Mobeto ambaye amezaa naye mtoto mmoja wa kiume aitwaye Dyllan na msanii wa muziki wa Kizazi Kipya nchini Kenya, Tanasha Donna ambaye naye amezaa naye mtoto mmoja wa kiume aitwaye Naseeb Junior.

 

 

Akizungumza na Gazeti la IJUMAA mapema wiki hii, Mama Dangote anasema kuwa, watu wengi wanafikiri yeye na Zari wana tatizo lolote au hawana mawasiliano mazuri, lakini ukweli ni kwamba, wanapendana sana na wanachati muda wowote.

 

 

“Ukitaja jina la Zari ujue huo ndiyo moyo wangu; tena amenizalia wajukuu wazuri wawili na tunachati sana.

“Yaani hakuna shida kabisa kati yangu mimi na Mama T (Mama Tiffah),” anasema Mama Dangote.

 

 

Akiendelea kuzungumza, Mama Dongote anasema kuwa, amekuwa akisikia watu wakisema ‘wameblokiana’ (mitandaoni), jambo ambalo si la kweli kwani hawawezi kufanyiana hivyo na ni marafiki wanaopenda.

 

 

“Mimi na Zari sidhani kama kuna hilo jambo la kublokiana; maana mimi ninachati naye huku WhatsApp kila siku, hata muda wa kuangalia huko Instagram sina kabisa miye, ila wajue Zari ndiye roho yangu, hivyo tu,” anasema Mama Dangote akimaliza kabisa ule uvumi wa mara kwa mara kuwa hana mawasiliano mazuri na mzazi mwenza huyo wa mtoto wake.

 

STORI: IMELDA MTEMA, DAR

Leave A Reply