The House of Favourite Newspapers

Mama Harmo Afunguka Simjui Kajala

0

HABARI ya mjini kwa sasa ni kapo mpya kabisa ya staa wa Bongo Fleva, Rajabu Abdul ‘Harmonize’ na muigizaji grade one wa Bongo Movies, Kajala Masanja, IJUMAA WIKIENDA lina ubuyu wao kama wote!

 

Ilianza kama masihara, Magazeti Pendwa ya Global Publishers yakawa ya kwanza kuripoti uhusiano wao angali ukiwa gizani na hatimaye wikiendi iliyopita, waliamua kujilipua na sasa siyo siri tena, wawili hao ni mtu na mtuwe.

 

MAMA HAJUI CHOCHOTE

Cha kushangaza sasa, wakati wenyewe wakijilipua, wakioneshana makopakopa kama yote Siku ya Valentine (Valentine’s Day), jana, mama mzazi wa Harmonize au Harmo, Habiba Chivala amesema kwa kinywa chake kwamba hamjui mkwewe huyo mpya.

 

Mama ni kama amepitwa hivi, mpaka sasa anajionea ‘mapichapicha’ tu, haelewi chochote kinachoendelea.

 

Picha linaanza mama hamjui Kajala na hata uhusiano huo ambao tayari umefikia kwenye hatua ya kuvalishana pete, bado mama mkwe wa Kajala, Bi Habiba hana taarifa.

BATA LA VALENTINE

Wikiendi iliyopita, Kajala akiwa ameambatana na ‘ubavu’ wake huyo, sambamba na watoto wao wa kufikia (Paula na Zhu), walitia nanga visiwani Zanzibar kusherehekea Sikukuu ya Wapendanao (Valentine’s Day) kwenye visiwa hivyo vya marashi ya karafuu.

UFAFANUZI KIDOGO

Paula ni mtoto wa Kajala aliyeza na Prodyuza maarufu Bongo, Paul Mathyyasse ‘P Funk’ huku Zhu akiwa ni mtoto wa Harmonize aliyezaa na mrembo anayefahamika kwa jina la Shanteel.

 

TURUDI KWA MAMA SASA…

Akizungumza na Gazeti la IJUMAA WIKIENDA kwa njia ya simu (exclusive), mama yake Harmo akiwa Tandahimba mkoani Mtwara, anasema kuwa, hajui chochote kinachoendelea na hata Kajala mwenyewe hamjui.

 

Anasema kuwa, anavyoulizwa kuhusu Kajala ni kama kumchanganya kwa sababu hafuatilii chochote cha mtandaoni kwa maana vingi havimuhusu na yeye ameshakuwa mtu mzima.

MAMBO YALIKUWA HIVI…

IJUMAA WIKIENDA: Shikamoo mama?

MAMA HARMONIZE: Marahaba vipi hali?

IJUMAA WIKIENDA: Unaongea na Mwandishi wa Gazeti la IJUMAA WIKIENDA kutoka Global, kuna madai sasa hivi Harmonize mpenzi wake ni Kajala na ndiye anataka kumuoa…una taarifa hizo?

 

MAMA HARMONIZE: Kajala ndiyo nani?

IJUMAA WIKIENDA: Mama humjui Kajala kweli?

MAMA HARMONIZE: Simjui kabisa na mimi siyo mtu wa mtandaoni, amefanyaje kwani?

IJUMAA WIKIENDA: Sasa hivi ndiye mkweo baada ya Sarah, huna habari mama?

MAMA HARMONIZE: Kwa kweli sijui hilo maana bado hajaniambia na mimi siyo mtu wa mitandaoni kabisa, wala kwenye vyombo vya habari na sijui lolote, labda mwenyewe anaweza kuzungumza.

IJUMAA WIKIENDA: Sawa mama asante.

MAMA HARMONIZE: Haya asante mwanangu.

Leave A Reply