The House of Favourite Newspapers

Mama Samia ampa kiwewe Sandra

0

sandra35Msanii wa filamu Bongo, Salama Salmini ‘Sandra.

Na Gladness Mallya
MAKUBWA! Msanii wa filamu Bongo, Salama Salmini ‘Sandra’ hivi karibuni alijikuta akipata kiwewe mbele ya Makamu wa Rais, Mama Samia Suluhu kwa kurudia kupiga naye picha zaidi ya mara mbili.

Ishu hiyo ilitokea wakati Mama Samia akiongoza kufanya usafi maeneo ya Kinondoni, Dar ambaye baada ya zoezi hilo, alipozi ili kupiga picha na wananchi mbalimbali waliojitokeza kuunga mkono wito wa Rais Magufuli wa kufanya usafi.

“Unajua picha kama hizi za kupiga na mtu muhimu kama huyu ni adimu sana, naweza nisipate nafasi hii tena ndiyo maana nimerudi mara kadhaa huku nikimuomba mtu anipige kwa simu yangu ya mkononi ili kuweka kumbukumbu vizuri,”alisema Sandra.

Leave A Reply