The House of Favourite Newspapers

Mama wa P Funk Azikwa Uholanzi

0

MWILI wa mama mzazi wa mtayrishaji wa muziki wa Bongo Fleva, P Funk Majani, Aunt Sheilah, umeshindikana kurudi ili kuzikwa Tanzania kwa sababu ya changamoto ya usafiri na janga la Corona, hivyo ulitarajiwa kuzikwa jana nchini Uholanzi.

 

Mwenyekiti wa kamati wa maandalizi wa msiba huo ambaye ni msanii Soggydogg Anter, jana alisema mwili huo utazikwa Uholanzi na P Funk mwenyewe yupo huko kwa ajili ya mazishi, ambapo atarejea Tanzania Ijumaa usiku na siku ya Jumamosi watafanya dua maalum kwa marehemu.

 

“Siku ya leo (jana) tunatarajia mwili wa mama mzazi wa P Funk Majani, Aunt Sheilah, kuzikwa nchini Uholanzi, imebidi azikwe huko kwa sababu usafiri ulikuwa mgumu na wenzetu bado wana wasiwasi na ugonjwa wa Corona.

 

“P Funk Majani mwenyewe tayari yupo huko kwa ajili ya mazishi na atarejea Tanzania siku ya Ijumaa usiku, kisha Jumamosi itafanyika dua ya marehemu nyumbani kwake Bamaga mahali ambapo zipo studio za Bongo Records,” amesema.

 

Marehemu alifariki nchini Uholanzi wakati akipatiwa matibabu siku ya Septemba 8, mwaka huu na taarifa kuhusu kifo chake zilitoka Tanzania siku ya Septemba 10.

Leave A Reply